Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumatatu hii, Wilson, Ake, Llorente, Fellain, Arnautovic, Willian, na wengine sokoni

Bournemouth iko radhi kumuuza mshambuliaji wa England Callum Wilson kwa Chelsea kwa pauni £75m – mara 25 zaidi ya kiwango walicholipa kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 mnamo 2014. (Star)

Wolves watapambana na Chelsea katika kuwania kumsajili Wilson, ambaye amefunga mabao 10 kufikia sasa msimu huu.(Birmingham Mail)

Chelsea pia inataka kumsajili upya beki wa kati wa Bournemouth Nathan Ake, miaka miwili tu baada ya kumuuza Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa Cherries. (Sun)

Uga mpya wa Tottenham inaarifiwa kwamba huenda usikamilike msimu huu. (Mail)

Mshambuliaji wa Tottenham na timu ya taifa ya Uhipania Fernando Llorente, mwenye umri wa miaka 33, analengwa na Barcelona. (Mundo Deportivo)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anasema klabu hiyo haitofikiwa kiwango kinachohitajika kumnunua mchezaji wa kiungo cha kati wa Wolves na Ureno Ruben Neves mwenye umri wa miaka 21 cha thamani kwa thamani ya £100m (Mirror)

Mshambuliaji wa Watford raia wa Ufaransa Abdoulaye Doucoure, aliye na miaka 26, ameiambia televisheni ya Ufaransa kwamba ‘ataondoka’ Hornets. (Canal Football Club, via Express)

Winga wa West Ham Michail Antonio anasema mchezaji mwenza wa Hammers na mshambuliaji wa Austria Marko Arnautovic, mwenye umri wa miaka 29, anataka kuelekea China. (Sky Sports)

Aliyekuwa winga wa Liverpool Ryan Babel, mwenye umri wa miaka 32, anakaribia uhamisho kwenda Fulham kwa mkopo. Raia huyo wa Uholanzi kwa sasa anaichezea Besiktas. (De Telegraaf)

Liverpool wanamfukuzia winga wa Celtic na Uskotchi James Forrest, aliye na miaka 27. (Scottish Sun)

Lille imejitosa katika kumwania mchezaji wa kiungo cha kati wa West Ham Pedro Obiang, aliye na miaka 26. Raia huyo wa Guinea ya Ikweta pia analengwa na Fiorentina. (RMC Sport)

Bournemouth itampa mkataba mpya mchezaji wa kati David Brooks, aliye na miaka 21, ili kuondosha matumaini kutoka kwa Manchester United na Tottenham. (Sun)

Fulham, Huddersfield na Leeds ni miongoni mwa vilabu vilivyo na hamu ya kumsajili mchezaji wa Columbus Crew na timu ya taifa ya Marekani Gyasi Zardes, aliye na miaka 27. (Teamtalk)

Leeds pia inapanga kumwania winga wa Wales Daniel James, aliye na miaka 21, na winga wa Ecuador Jefferson Montero, mwenye miaka 29, ambao wote wanaichezea timu ya Swansea.(Sun via Wales Online)

Leeds pia inawania kukamilisha usajili wa kipa wa Southampton Fraser Forster, mwenye umri wa miaka 30, kufikia mwishoni mwa wiki (Star)

Manchester United inamtaka mlinzi wa Uholanzi Timothy Fosu-Mensah asalie kwa mkopo Fulham lakini timu hiyo inataka mchezaji huyo wa miaka 21 aondoke ili ipokee wachezaji zaidi kwa mkopo. (Sun)

Aliyekuwa mchezaji wa Manchester United Andy Cole anatarajiwa kujiunga na Sol Campbell huko mjini Macclesfield kama kocha wa washambuliaji wa timu hiyo. (Mail)

Manchester United wanatafakari uwezekano wa kumuajiri meneja wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate huku kampeini ya kumtafuta mrithi wa Jose Mourinho ikiendelea. (Sunday Telegraph)

Meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone, ambaye mkataba wake na klabu hiyo ya Uhispania unakamilika miezi 18 ijayo pia yuko katika orodha ya meneja mpya wa United. (Sunday Mirror)

Inter Milan wanapigiwa upatu kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Ecuador. (Sunday Mirror)

AC Milan wanajiandaa kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United na timu ya taifa ya Ubelgiji Marouane Fellaini, 31. (Mail on Sunday)

Chelsea wanamfuatilia kiungo wa kati wa Paris St-Germain Adrien Rabiot.

Kiungo huyo wa miaka 23 raia wa Ufaransa pia analengwa na Barcelona. (L’Equipe – in French)

Juventus wamekataa ofa ya Chelsea ya kubadilishana Alvaro Morata na Gonzalo Higuain. (Calciomercato)

Kiungo huyo wa miaka 30 pia anatafutwa na Barcelona. (Sunday Mirror)

Manchester City wanatafakari uwezekano wa kumsajili Allan, 28 ambaye ni kiungo wa kati wa Napoli na Brazil. (Tuttomercato – in Italian)

Kuna uwezekano wa Arsenal kumpatia Suarez mkataba wa kudumu (Mundo Deportivo – in Spanish)Winga wa Chelsea na Brazil Willian analengwa na klabu ya Dalian Yifang inayoshiriki ligi kuu ya Uchina.

Chanzo BBC

By Ally Juma.


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents