Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumatatu hii, Zidane, Dembele, Alderweireld, Icardi, Werner, Zaniolo, Pepe na wengine sokoni

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema kuwa klabu hiyo huenda ikawauza wacheza muhimu mwisho wa msimu huu. Raia huyo wa Ufaransa anataka kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake baada ya msururu wa matokeo mabaya msimu huu.. (Sky Sports)

REAL MADRID – ACF FIORENTINA

Manchester United hawana hamu na mshambuliaji wa zamani wa Lyon Moussa Dembele.

mshambuliaji wa zamani wa Lyon Moussa Dembele.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amefunga magoli 18 katika mashindano yote msimu huu. (Mirror)

Arsenal wanataka kumsaini beki wa Tottenham na Ubelgiji Toby Alderweireld, 30. (Talksport)

Mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi anatarajiwa kuondoka Inter Milan msimu huu.

beki wa Tottenham na Ubelgiji Toby Alderweireld,

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 huenda akahamia Real Madrid kwa dau la £52m. (AS)

Mchezaji anayelengwa na Liverpool na Bayern Munich Timo Werner hatotia saini kandarasi mpya na klabu ya RB Leipzig.

Kandarasi ya mshambuliaji huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 23 katika klabu hiyo ya Bundesliga inakamilika mwisho wa msimu huu. (Sky Germany)

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund 19 na Sweden Alexander Isak

Chelsea itashindana na Real Madrid katika mbio za kumnunua ,mshambuliaji wa Borussia Dortmund 19 na Sweden Alexander Isak. (Sun)

Hatahivyo Zidane mwenye umri wa miaka 46 amepinga madai kwamba atamuuza mshambuliaji wa Ufaransa Karim Benzema, 31. (Marca)

Na timu hiyo itamuuza beki wa Ufaransa Raphael Varane, 25, kwa dau la £437m kutokana na sheria inayomzuia katika kandarasi yake . (RAI Sport via Calciomercato)

Beki wa Ufaransa Raphael Varane, 25

Bayern Munich wanamtaka kiungo wa kati wa Roma na Itali Nicolo Zaniolo mwenye umri wa miaka 19. (Bild – in German)

Rais wa klabu ya Lille Gerard Lopez anasema kuwa winga wa Ivory Coast ,23, Nicolas Pepe, ambaye ananyatiwa na Manchester United, ataondoka katika klabu hiyo ya Ufransa mwisho wa msimu huu . (Manchester Evening News)

Leicester imewachukua vijana watatu ili kusaidia kuendeleza timu hiyo katika siku za usoni.

Bruno Fernandes

Kiungo wa kati wa Guiseley Dylan Barkers, Beki wa Hasting United Jamie Fielding na kiungo wa kati wa Hasting Adam Lovatt wamejiunga na klabu hiyo. (Leicester Mercury)

Wawakilishi kutoka Manchester United, Juventus na Paris St-Germain walizuru klabu ya Aves ili kumtazama kiungo wa kati wa Sporting Lisbon ,24, Bruno Fernandes. (A Bola)

Kundi moja la wafanyibiashara linaloungwa mkono na European Money liko tayari kuinunua klabu ya Huddersfiedl Town kwa kitita cha £50m. (star)

Ole Gunnar Solksjaer
Image captionKocha wa Manchester United Ole Gunnar Solksjaer

Klabu ya Manchester United kumpatia kocha wao Ole Gunnar Solksjaer pauni milioni 200 za usajili. Hiko ndiyo kiwango kikubwa zaidi United kuwahi kutoa. (Sunday Express)

Kiungo Paul Pogba, 26, anatarajiwa kupewa unahodha katika klabu yake ya Manchester United ili kuzima mipango ya kuhamia Real Madrid. (Sunday Mirror)

Manchester United watachuana na mahasimu wao Manchester City katika mbio za kumsajili beki kinda wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England Aaron Wan-Bissaka, 21, mwenye thamani ya pauni milioni 40. (Mail on Sunday)

Miamba hiyo ya Old Trafford club pia ipo tayari kumlipa mshahara mara tatu ya anaopokea sasa kiungo Christian Eriksen, 27, wa Tottenham endapo atakubali kujiunga nao mwishoni mwa msimu.

Eriksen
Image captionChristian Eriksen

Man united pia wanaendelea kumnyemelea beki wa Napoli Kalidou Koulibaly. Beki huyo raia wa Senegal mwenye miaka 27 ana thamani ya pauni milioni 110. (Sunday Express)

Kiungo wa Arsenal na Uswizi Granit Xhaka, 26, ananyemelewa na miamba ya soka nchini Italia klabu ya Inter Milan.(Sunday Express)

Barcelona wanatazamiwa kujaribu kumsajili tena winga wa Chelsea Willian, 30. Barca waliwahi kupeleka dau la pauni milioni 55 ili kimsajili Mbrazili huyo lakini wakakataliwa. (Sunday Telegraph)

Tottenham wanamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Celta Vigo na Uruguay Maxi Gomez. Gomez 22- mkataba wake una thamani ya pauni milioni 43. (Mail on Sunday)

Dybala
Image captionPaulo Dybala wa Juventus

Juventus watalazimika kumuuza mshambuliaji wao Paulo Dybala, 25, ili kuwezesha kupata pauni milioni 86.4 ili wamsajili mshambuliaji wa Benfica Joao Felix, 19. (Tuttosport via Football Italia)

Rais wa Benfica Luis Filipe Vieira wiki iliyopita alikataa dau la pauni milioni 65 kutoka kwa miamba hao wa Italia. (O Jogo – in Portuguese)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents