Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya, Leroy Sane hatiani kutia saini Man City, Mkhitaryan aeleza kukosa raha ligi ya Uingereza

Tetesi za usajili barani Ulaya, Leroy Sane hatiani kutia saini Man City, Mkhitaryan aeleza kukosa raha ligi ya Uingereza

Manchester City inajaribu kumshawishi mshambuliaji wake Leroy Sane, 23, kutia saini kandarasi mpya kabla ya Bayern kupewa fursa nyengine ya kuwasilisha ombi la kumsaini raia huyo wa Ujerumani . (Standard)

Chelsea itajaribu kumsaini beki anayedaiwa kuwa na thamani ya £35m kutoka klabu ya Nice Youcef Atal, raia wa Algeria mwenye umri wa miaka 23 mwezi Januari iwapo watafanikiwa kuondolewa marufuku yao ya uhamisho kuanzia mwanzo wa 2020. (Sun)

Manchester United inamnyatia kiungo wa kati wa Benfica na Portugal Florentino Luis, 21, lakini anaweza kukabiliwa na ushindani wa kumsaini kutoka kwa klabu ya Manchester City (A Bola via Sport Witness – in Portuguese)

Florentino Luis,Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Kiungo wa Real Betis na Ufaransa Nabil Fekir, 26, amekana madai kwamba uhamisho wake wa dau la £53m kuelekea Liverpool 2018 uligonga mwamba kutokana na kufeli kwa vipimo vya matibabu.. (L’Equipe, via Talk Sport)

Manchester City ilifeli katika ombi lake la kumsaini beki wa inter Milan raia wa Slovakia Milan Skriniar, 24, lakini inaweza kujaribu tena mwezi Januari. (Tuttosport, via Sport Witness)

Kiungo wa kati wa Armenia ambaye aliwahi kuzichezea Manchester United na Arsenal Henrikh Mkhitaryan, 30, ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Roma amesema kwamba kipindi chake cha mchezo katika ligi ya Premia kilimfanya kukosa mapenzi na kandanda. (Manchester Evening News)

Henrikh Mkhitaryan

Chelsea itajaribu kumsaini beki wa kushoto wa Valencia na Uhispania Jose Gaya, 24, wakati marufuku ya dirisha la uhamisho itakapokamilika msimu ujao. (Soccer Link, via Talk Sport)

Beki wa zamani wa Arsenal na Ujerumani Per Mertesacker, 34, anaamini wachezaji wa klabu hiyo walishindwa kutoa ushahidi wa kuwepo kwa imani ya Wenger katika siku za mwisho za mkufunzi huyo wa zamani wa Arsena(Standard)

Kiungo wa kati wa Brazil Lucas Piazon, 25, anasema yuko tayari kuondoka Chelsea kabisa kwa kuwa amechoshwa na hatua ya kuuzwa kwa mkopo kila mwaka. (A Bola, via Goal)

Lucas Piazon

Arsene Wenger anasema kwamba majuto yake makubwa akiifunza Arsenal ni kushindwa kumsaini mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi. (beIN Sports)

Mkufunzi wa taasisi ya soka ya Crystal Palace Shaun Derry amefichua jinsi siku nne za kuichezea klabu ya Cambridge United zilivyomfanya beki wa England Aaron wan Bissaka kushawishika kuanza safari yake kuelekea Man United. . (Standard)

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents