Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya, mashabiki wa PSG wamsusa Neymar, Pogba matatani

Tetesi za usajili barani Ulaya, mashabiki wa PSG wamsusa Neymar, Pogba matatani

Wawakilishi wa kisheria wa mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Paris St-Germain, Neymar ,27, walionekana wakiingia katika ofisi za klabu yake ya zamani Barcelona. (Gol TV, via AS). Real Madrid imeendelea kuwa na nia ya kumsajili Neymar na kutamatisha nia ya kumsajili kiungo wa Manchaster United Paul Pogba, 26, ikiwa watampata mchezaji huyo. (Sun)

PSG imeonekana kusitisha kuuza shati la Neymar kwenye duka la klabu. (UOL Esporte, via Marca). Manchester United wameshtushwa na taarifa kuwa Pogba anaweza kuachana na klabu hiyo. (Mirror)

Paul PogbaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mabingwa wa Italia Juventus imezungumza na kiungo Christian Eriksen, 27, wakimtaka kujiunga na timu hiyo mkataba wake na Tottenham utakapomalizika mwishoni mwa msimu.(Mail)

Bayern Munich wako kwenye mazungumzo na Barcelona kuhusu usajili wa kiungo wa Brazil Philippe Coutinho, 27, kwa mkopo. (RAC1, via AS).

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Daniel Sturridge, 29, atafanya maamuzi kuhusu mustakabali wake juma hili wakati ambapo klabu 13 zimeonesha nia ya kumnyakua, huku klabu ya Uturuki Fenerbahce ikitangaza dau la pauni 60,000 kwa wiki. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, alikubali kuweka kando tofauti yake na uongozi wa Crystal Palace baada ya mchezaji mwenzake Mamadou Sakho kumtaka ajitume walipokuwa kwenye mkutano wa wachzaji. (Sun)

Bale (kushoto) alikuwa anajiandaa kujiunga na klabu ya Jiangsu Suning ya China mwezi JulaiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 30 ataendelea kubaki Real Madrid akisubiri dirisha la usajili la ligi ya China kufunguliwa mwezi Novemba au kocha Zinedine Zidane afukuzwe kazi. (Mail)

Inter Miami itamsajili mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 32, mkataba wake na PSG utakapokwisha mwezi Juni mwaka 2020. (Fox Deportes – in Spanish)

Dejan LovrenHaki miliki ya pichaREUTERS

Liverpool itakubali ofa ya pauni milioni 13.9 na marupurupu kwa ajili ya beki wa kati Dejan Lovren, 30, baada ya AC Milan na Roma kumtaka mchezaji huyo. (Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Sevilla na timu ya taifa Ufaransa Wissam Ben Yedder, 29, anatarajia kujiunga na klabu ya Monaco kwa kitita cha pauni milioni 37.1. (L’Equipe – in French)

Winga wa Ivory Coast Nicolas Pepe, 24, alijiunga na Arsenal akitokea Lille kwa sababu alitaka kujiunga na klabu ambayo angeweza kuipa faida kubwa , amesema raisi wa klabu ya Ufaransa.(Sky Sports)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents