Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya Moura, Dier, Haaland, Pogba na sokoni Zidane aanza kujitetea

Tetesi za usajili barani Ulaya Moura, Dier, Haaland, Pogba na sokoni Zidane aanza kujitetea

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Tottenham Lucas Moura, mwenye umri wa miaka 27, na mchezaji wa kiungo cha kati Eric Dier, aliye na miaka 25, wapo juu kwenye orodha ya Manchester United ya wachezaji wanaolengwa kwa uhamisho. (Star)

Inaarifiwa Manchester United ina hamu ya kumsajili meneja wa Paris St-Germain Thomas Tuchel kama anayewezekana kuichukua nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer iwapo matokeo hayatoimarika (Mail)

Wakati huo huo, Manchester United ina hamu ya kujadili kuongezwa muda kwa mkataba wa mchezaji wa kiungo cha kati anayeichezea timu ya taifa ya Ufaransa pia Paul Pogba na wakala wa mchezaji huyo wa miaka 26, Mino Raiola katika wiki chache zijazo. (ESPN)

Hatahivyo Meneja Solskjaer ana hamu ya kutomuuza Pogba kwenda Real Madrid. (Mirror)

Meneja Solskjaer ana hamu ya kutomuuza Pogba kwenda Real Madrid.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMeneja Solskjaer hataki kuumuza Pogba kwenda Real Madrid.

Arsenal inatumai kumsajili upya mchezaji wa kiungo cha mbele wa Uholanzi Donyell Malen, baada ya kufunga mabao 10 katika mechi 13 msimu huu kwa timu ya PSV Eindhoven. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 aliyeuzwa na Gunners kwa £500,000 miaka miwili iliyopita analengwa pia na timu ya Liverpool. (Mirror)

Wakati huo huo , meneja wa Arsenal Unai Emery ametoa wito wa subra kwa mashabiki wakati akijitahdi kupata matokeo mazuri kutoka kwa mchezaji aliyemsajili winga wa Ivory Coast , Nicolas Pepe, mwenye umri wa miaka 24. (Express)

Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema “hana wasiwasi” kuhusu uvumi kwamba aliyekuwa bosi wa Manchester United na Chelsea Jose Mourinho huenda akaichukua nafasi yake katika timu hiyo ya ligi ya Uhispania – La Liga. (Sun)

Video: Kipa wa Ujerumani Muhammet Sozer afunga bao la ajabu dhidi ya Uingereza

Zidane pia amedai kwamba kushindwa kwa Real Madrid kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Tottenham Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 27, na mchezaji wa kiungo cha kati wa Ajax Donny van de Beek, aliye na umri wa miaka 22, msimu huu wa mjira wa joto ni uamuzi wa bodi na sio wake binfasi. (Sun)

Crystal Palace, Leicester City na Middlesbrough ni miongoni mwa timu zilizo na hamu ya kumsajili beki wa kati wa Wolves Cameron John, mwenye miaka 20, ambaye anacheza kwa mkopo huko Doncaster Rovers. (Mail)

ZidaneHaki miliki ya pichaREUTERS

Inaarifiwa Juventus imejiunga katika kinyanganyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Red Bull Salzburg Erling Braut Haaland, mwenye umri wa miaka 19. Manchester United na Manchester City pia wana hamu ya kumsajili mchezaji huyo aliyefunga hat-trick katika ushindi wa 6-2 wa timu yake katika mechi ya ligi ya mabingwa dhidi ya Genk mapema wiki hii. (Mirror)

Aston Vila ipo tayari kushindana na Leeds United kumsajili mlinzi wa Coventry City Sam McCallum, mwenye umri wa miaka 19. (Birmingham Mail)

Huku dirisha la uhamisho likiwa limefungwa, Mkuu wa Bristol City, Lee Johnson amesema anaweza kuangalia usajili wa maajenti walio huru kufuatia jeraha la muda mrefu la goti la mshambuliaji anayecheza kwa mkopo kutoka Stoke City striker Benik Afobe, mwenye umri wa miaka 26. (Bristol Post)

Chanzo BBC.

By Allyu Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents