Aisee DSTV!

Tetesi za usajili barani Ulaya, Mourinho aikataa ofa ya kwenda China, Matthijs de Ligt njia panda Juventus Chelsea kumbakisha Hudson-Odoi darajani

Tetesi za usajili barani Ulaya, Mourinho aikataa ofa ya kwenda China, Matthijs de Ligt njia panda Juventus, Chelsea kumbakisha Hudson-Odoi

Winga wa Chelsea na England Callum Hudson-Odoi, 18, anakaribia kutia saini mkataba mpya na klabu hiyo, Stamford Bridge. (Goal). Manchester United wanajianda kuweka dau la kumnunua kiungo wa safu ya kati wa Newcastle Muingereza Sean Longstaff, 21. (Sky Sports)

Manchester United na Paris St-Germain zimekubaliana malipo ya kumnunua mlinzi wa Ajax na Uholanzi Matthijs de Ligt, 19. (European football expert Julien Laurens, via Express)

Tottenham inakaribia kukamilisha mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Real Madrid na Uhispania Dani Ceballos, 22. (AS)

Dani CeballosHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionDani Ceballos (aliyeinua mikono juu)

Arsenal huenda ikamsaini winga wa Uhispania Lucas Vazquez, 28, kwa mkataba wa pauni milioni 31 kutoka Real Madrid wiki ijayo. (AS)

Leicester inaelekea kuvunja rekodi ya uhamisho wa wachezaji kumsajili kiungo wa kati wa Monaco na Ubelgiji Belgium Youri Tielemans,22, ambaye aliyecheza kwa mkopo, uwanja wa King Power karibu nusu ya msimu uliyopita. (Leicester Mercury)

Liverpool pia wako tayari kumsaji Ceballos baada ya kutathmini kwa kina mpangao wao. (Sportwitness)

Cristian CeballosHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionCristian Ceballos (kushoto)

Mshambuliaji wa Bournemouth na England Callum Wilson, 27, ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa West Ham msimu ujao. (90Min)

Hammers wamewasilisha ombi la kutaka kumnunua mshambulizi wa Celta Vigo na Uruguay Maxi Gomez,24, ambaye pia ananyatiwa na Valencia.(Evening Standard)

Kocha wa zamani wa Manchester United na Chelsea Jose Mourinho amekataa ofa ya kuwa meneja wa klabu ya Guangzhou, ya China. (Guardian)

Jose MourinhoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJose Mourinho,Kocha wa zamani wa Manchester United

Spurs wanamtaka kiungo wa kati wa Roma na Italia Nicolo Zaniolo, 20. (Sportslens)

Kipa wa Newcastle United, Muingereza Karl Darlow, 28, analengwa na Blackburn Rovers. (Sky Sports)

Birmingham City wako tayari kupatia ofa ya majaribio mshambuliaji wa Stoke City, Saido Berahino,25. (Sun)

Saido BerahinoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSaido Berahino

Mabingwa wa Uturuki Galatasaray wanataka kumsajili mshambuliaji wa Italia Stefano Okaka, 29. (Watford Observer)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW