Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya, Tottenham kuipiku United kwa Dybala, Coutinho kutua Arsenal

Tetesi za usajili barani Ulaya, Tottenham kuipiku Man United kwa Dybala, Coutinho kutua Arsenal kwa mkopo

Tottenham wamefikia makubaliano na Juventus kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 25, kwa dau la karibu £62m. (Sky Sports Italia, via Daily Mail) Dybala anajiandaa kuanza mazungumzo ya mkataba na Tottenham kabla ya Alhamisi ambao ni muda wa mwisho uliowekwa kwa uhamisho wa wachezaji kukamilika. (Goal)

Tottenham pia wanapania kumsaini mshambuliaji wa Barcelona wa miaka 27- Mbrazil Philippe Coutinho. (ESPN

DC United wanajiandaa kufanya mazungumzo na wawakilishi wa kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 30, wanapojaribu kujaza pengo lililoachwa wazi na Wayne Rooney anayeelekea Derby. (Mirror)

Philippe Coutinho points to his ears after scoring against Manchester UnitedHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Manchester United wameongeza juhudi ya kufikia mkataba na na kiungo wa kati Tottenham Christian Eriksen, 27. (Telegraph)

Eriksen hayuko katika mpango wa wa muda mrefu wa Mauricio Pochettino, Tottenham – na tayari amethibitisha kuwa anataka changamoto mpya. (Mirror

Uamuzi wa dakika za mwisho wa United kumhusu Eriksen unakuja licha ya tetesi ikiwa kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, ataendelea kuwa katika klabu hiyo hadi mwisho wa dirisha la uhamisho litakapofungwa. (Standard)

Tottenham midfielder Christian EriksenHaki miliki ya pichaBBC SPORT

United pia wanawatarajiwa kufanya uamuzi ambao haukutarajiwa kumnyakua mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Fernando Llorente, ambaye kwa sasa yuko huru kuondoka klabu hiyo bila malipo. (Sky Sports Italy, via Metro

Manchester City wanatarajiwa kuthibitisha usajili wa Joao Cancelo kutoka Juventus siku ya Jumatano baada ya beki huyo wa miaka 25 raia wa Ureno kupita vipimo vya kimatibabu. (Star)

Liverpool hawana mpango wa kumuuza kiungo wa kati wa Brazil Fabinho, licha ya tetesi zinazomhusisha mchezaji huyo wa miaka 25 na uhamisho wa Real Madrid. (Echo)

FabinhoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Crystal Palace wamekataa ofa ya £70m kutoka kwa Everton kumnunua mshambuliaji wa Ivory Coast forward Wilfried Zaha, 26.

Everton ilikuwa imewajumuisha wachezaji kama vile mshambuliaji wa Uturuki Cenk Tosun, 28, na kiungo wa kati wa Jamhuri ya Ireland James McCarthy, 28, katika ofa hiyo. (Mail

Lakini Palace wanakaribia kufikia mkataba wa kumsajili McCarthy kutoka Everton kwa hadi £8.5m. (Sky Sports)

Wilfried ZahaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionZaha amaeifungia Place mabao 10 msimu wa 2018-19

Paris St-Germain imetoa ofa ya kumnunua mchezaji nyota wa Brazil Neymar, 27, kwa vilabu vya Manchester United, Juventus na Real Madrid.

Vilabu hivyo vinafanya kila juhudi kuhakikisha Barcelona haimsajili tena mchezaji wao wa zamani. (Sport

Lukaku kwa mara nyingine amefanya mazoezi na na wachezaji wa chini ya miaka 18 wa Anderlecht siku ya Jumanne, bila idhini ya United kuwa mjini Brussels. (Mail)

Manchester United forward Romelu LukakuHaki miliki ya pichaREUTERS

Mshambuliaji wa Manchester United raia wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, hajarejea kutoka Carrington kujiunga na mazoezi ya kikosi cha kwanza licha ya tetesi zinazohusiana na hatma yake ya baadae katika katika klabu hiyo. (Mirror)

Everton wanakaribia kumsaini kwa mkopo beki wa Monaco Mfaransa Djibril Sidibe, 27. (Mail)

NeymarHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Manchester United na Manchester City wametuma wataalamu wao kufuatilia mchezo wa kiungo wa kati wa Norway Hakon Evjen ,19 wakati wa mchuano wa Bodo/Glimt. (TV2 via Manchester Evening News)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents