Tia Kitu. Pata Vituuz!

Tetesi za usajili Juma hili na klabu kubwa barani Ulaya namna zinavyo haha kusaka saini za nyota hawa 

Barcelona inamnyemelea mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang, 30 ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu ujao. (Sunday Express)

Arsenal

Nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo, 35, amesema kwamba anafurahia kuwa Juventus na hana nia ya kujiunga na Inter Miami inayomilikiwa na David Beckham. (Sky Sports)

Grealish is a lifelong Villa supporter who was born in Birmingham and joined the club aged six

Grealish amekuwa shabiki wa Villa karibu maisha yake yote. Alizaliwa Birmingham na kujiunga na klabu hiyo akiwa na miaka 6

Manchester United wako tayari kutoa kima cha paundi 150,000 kwa wiki kwa nahodha wa Aston Villa Jack Grealish ili kuwa Old Trafford katika msimu ujao wa uhamisho. (Sun)

Chelsea imeungana na Liverpool, Manchester United na Tottenham katika kufuatilia maendeleo ya mshambuliaji -Jonathan David ambaye thamani take inasemekana kuwa £20m. Mchezaji huyo, 20, aliifungia timu yake ya Ubelgiji magoli 23 msiku huu. (Sunday Express)

Liverpool itakuwa na kibarua cha kuimarisha upande wa kushambulia msimu ujao kwasababu mchezaji wa kimataifa Adam Lallana, 31, na Xherdan Shaqiri, 28, wa Switzerland wote wanatarajiwa kuondoka mwisho mwa msimu. (The Athletic via Express)Abdoulaye Doucoure

Abdoulaye Doucoure mchezaji wa Watford

Kiungo wa kati wa Watford Abdoulaye Doucoure, 27, anstahili kuwa mlengwa mzuri wa Liverpool, kulingana na aliyekuwa mchezaji wa kimataifa Owen Hargreaves. (Daily Star)

Manchester City italazimika kulipa £40m ikiwa inataka kumsajili mlinzi wa Everton Mason Holgate, 23. (Football Insider)

Mshamambuliaji wa Borussia Dortmund, Erling Braut Haaland ndo anayependelewa na Real Madrid wakati inapojiandaa kuongeza mshambuliaji mwengine kwa msimu wa tatu mfululizo. Timu hiyo ya Uhaspania inafahamu kwamba itahitajika kulipa takriban £65m kwa mchezaji huyo, 19, wa Norway. (Marca, in Spanish)

Werner, centre, scored from the penalty spot against Tottenham on WednesdayWerner, katikati, alipata goli kwa penalti dhidi ya Tottenham

Mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner, 23, pia yuko kwenye orodha ya Real Madrid na kumaanisha kwamba huenda Liverpool ikapata upinzani wa kumpata mchezaji huyo wa Ujerumani anayesemekana kuwa na thamani ya £51. (Daily Mail)

Kocha wa Sheffield United Chris Wilder anasema kiungo wa kati John Fleck, aliyetia saini kandarasi mpya wiki iliyopita, alikuwa anawindwa na timu nyengine. Mchezaji huyo, 28, amehusihwa kuhamia Arsenal. (Sheffield Star)

Ugurcan Cakir
Ugurcan Cakir

Kitita cha £11m kilichokuwa kimependekezwa na ”The Blades” kwa klabu ya Trabzonspor ya Uturuki kama jitihada za kutaka kumsaini Ugurcan Cakir, 23, anayesemekana kwamba tahamani yake ni ya juu zaidi zimekataliwa mbali. (Fotosport via Sun)

Mchezaji wa kimataifa Cakir, ambaye pia kuna tetesi kwamba ana mezewa mate na Liverpool, Everton na Manchester United, huenda gharama ya kumsajili ikaongezeka hadi £26m na anaorodheshwa kuwa mmoja kati ya walinda lango watatu wazuri duniani na rais wa klabu ya Trabzonspor, Ahmet Agaoglu. (Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford ana imani kubwa kwamba ataweza kurejea uwanjani kabla ya mwisho wa msimu huu kutokana na jeraha la mgongoni.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW