Michezo

Tetesi za usajili Simba, Yanga, Azam na klabu nyingine Bongo

Tetesi zilizopo kwenye sajili za soka nchini Tanzania zinadai kuwa Miamba ya soka Ligi Kuu Tanzania Bara na Mabingwa wa Nchi #simbasc wamemsaini kinda wa miaka 19 raia wa Congo kiungo wa klabu ya DC Motema Pembe, Karim Kiekie Kamvuidi.

Karim kwa sasa yuko Cameroun na timu ya Taifa ya Congo DR kwenye mashindano ya CHAN. Kwenye mchezo wa timu yake ya taifa na Tanzania Taifa Stars alivalia jezi namba 17.

Wakati Mnyama Simba akiwa mbioni kutafuta mbadala wa Sven, inadaiwa mabingwa hao watetezi Ligi Kuu wamefanya mazungumzo na kocha wa zamani wa Klabu ya Pyramids ya nchini Mirsi, Sebastian Desbare ili kuja kurithi mikoba ya Sven Vanderbroek aliyeondoka baada ya kuivusha Simba hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Barani Afrika.

Yanga imefanikiwa kumsajili, Fiston Abdulrazaq ambaye walimtangaza mapema mwanzoni mwa wiki hii na hawa ndiyo waliyosajiliwa mpaka sasa dirisha dogo Said Ntibazonkiza – Mshambuliaji, Fiston Abdulrazaq – Mshambuliaji na Dickson Job – Beki.

Mnyama yupo mbioni kukamilisha usajili wa beki kutoka Zimbabwe, Peter Muduwa mwenye umri wa miaka 27 anayekipiga kwenye Klabu ya Highlanders ambaye kwa sasa yuko CHAN.

Azam FC imefanikiwa kumrejesha mshambuliaji Yahya Zayd mwenye umri wa miaka 24 akitokea klabu ya Pharao FC kutoka nchini Misri. Inadaiwa Zayd amejiunga na Wanarambaramba hao kwa kandarasi ya miezi sita na nusu.

Inaelezwa kuwa kiungo wa klabu ya Yanga, Haruna Niyonzima ndiye mchezaji wa kigeni aliyecheza kwa muda mrefu zaidi nchini Tanzania.

Tetesi zilizopo kwenye mitandao ya kijamii zinadai kuwa klabu ya Simba imepanga kumpa mkono wa kwaheri kiungo raia wa Kenya, Fransis Kahata mwishoni mwa msimu huu mkataba wake utakapomalizika.

Taarifa zisizo rasmi zinadai kuwa Simba SC imemnasa mshambuliaji Junior Lukosa kutoka Nigeria katika harakati za kuhakikisha inajiimarisha vema na michuano inayowakabili.

IMEANDIKWA NA Hamza Fumo Instagramu @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents