Aisee DSTV!

Tetesi za usajili Ulaya leo, Sarri kutimkia Juventus, De Light bado kidogo tu United, mazungumzo ya Madrid na Chelsea kuhusu Hazard yapamba moto, hazard aonekana Uhispania, Eriksen, Pogba, Mane, Ozil na wengine sokoni

Tetesi za usajili Ulaya leo, Sarri kutimkia Juventus, De Light bado kidogo tu United, mazungumzo ya Madrid na Chelsea kuhusu Hazard yapamba moto, hazard aonekana Uhispania, Eriksen, Pogba, Mane, Ozil na wengine sokoni

Mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri amekubali kuwa mkufunzi mpya wa Juventus na ameitaka Chelsea kumruhusu kuondoka.(Goal). Sarri alimuelezea Marina Granovskaia kuhusu uamuzi wake katika mkutano siku ya Ijumaa na mkurugenzi huyo wa Chelsea aliahidi kuzungumzia hatma yake na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich. (Sky Italy – in Italian)

Chelsea inasubiri hatua rasmi kutoka kwa mabingwa hao wa Juventus , ambao watalazimika kulipa kandarasi yake ya mwaka mmoja yenye thamani ya £5m. (Guardian).

Uwanja wa BakuHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mamlaka mjini Baku iliagiza kufunguliwa kwa milango katika uwanja huo katika kipindi cha kwanza cha mechi ya fainali ya kombe la ligi ya Europa dhidi ya Arsenal na Chelsea kwa kuwa waliaibishwa na ukosefu wa mashabiki katika uwanja huo.(Times – subscription required)

Beki wa Ajax Matthijs de Ligt, 19, ataipatia Man United uamuzi wa uwezekano wa kuhamia katika klabu hiyo ya Old Trafford katika siku chache zijazo. (Telegraph)

Beki wa Ajax Matthijs de Ligt

Manchester City inamnyatia kiungo wa kati wa Ufaransa na Lyon mwenye umri wa miaka 22 Tanguy Ndombel epamoja na kiungo wa kati wa Uhispania Marco Llorente, 24, kama mchezaji mbadala iwapo watashindwa kumsajili kiungo wa kati wa Atletico Madrid na Uhispania Rodri, 22. (Manchester Evening News)

Ilkay Gundogan atasalia katika klabu ya Manchester City msimu ujao hata iwapo kiungo huyo wa Ujerumani ,28, atakuwa ajenti huru wakati ambapo kandarasi yake itakamilika mwisho wa msimu huu.(Mail)

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane amezuia kuondoka kwa beki wa Uhispania Sergio Ramos, 33, . (ESPN)

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane amezuia kuondoka kwa beki wa Uhispania Sergio RamosHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Real imesitisha harakati zao za kumsaka mshambuliaji wa Benfica mwenye umri wa miaka 19 raia wa Ureno Joao Felix ili kuimarisha juhudi za kuweza ikumsajili mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard. (Marca)

Rial Madrid wanatarajiwa kufanya mazungumzo na Chelsea ili kujadiliana kuhusu usajili wa Eden hazard. (Mail)

kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen

Na Real itamuwania kiungo wa kati wa Ajax na uholanzi Donny van de Beek, 22, ama kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27, iwapo itashindwa kumpata kiungo wa kati wa man United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Sun)

Wakati huohuo , Juventus inamlenga kinda wa klabu ya Empoli kutoka Ivory Coast Hamed Traore kama mchezaji mbadala wa Pogba. (Calciomercato)

Arsenal na Leicester wanamchunguza winga kinda wa Valencia Uhispania Ferran Torres,19, ambaye ana thamani ya £25m. (Mail)

Mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane

Mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane, 27, anasema alikaribia kujiunga na Man United baada ya kuzungumza na mkufunzi Louis van Gaal, kabla ya simu ya Jurgen klopp kubadili mafikra yake.. (Mirror)

Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery yuko tayari kumuuza kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, 30, mwisho wa msimu huu (Standard)

The Gunners wamewasiliana na Leicester kuhusu uwezekano wa kumsaini kiungo wa kati wa klabu hiyo James Maddison lakini wamedaiwa kutaka kulipwa £60m. (Mail)

James MaddisonHaki miliki ya pichaREUTERS

Barcelona ni miongoni mwa klabu zinazompigania mshambuliaji wa klabu ya Girona raia wa Uruguay 32 Cristhian Stuani, ambaye aliichezea Middlesbrough. (Marca)

Kipa wa Barcelona na Uholanzi Jasper Cillessen, 30, ameikosoa klabu hiyo kwa kuweka dau la £53million huku klabu ya Man United na Benfica zikivutiwa na mchezaji huyo. (Mail)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW