Tupo Nawe

Tetesi za usajili Ulaya: Manchester United wamgeukia Zlatan, Liverpool yamsaka N’golo Kante kwa nguvu zote

Tetesi za usajili Ulaya: Manchester United wamgeukia Zlatan, Liverpool yamsaka N'golo Kante kwa nguvu zote

Manchester United wameweka wazi kuwa kumsajili mshambuliaji ni kipaumbele katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari na wameelekeza macho yao kwa mshambuliaji wao wa zamani Zlatan Ibrahimovic, 38. (Daily Express)

 

Timu hiyo ya Old Trafford pia inampa nafasi ya juu kumsajili kiungo wa West Ham Declan Rice 20, ifikapo Januari, lakini huenda ikawagharimu pauni milioni 80. (Goal via Mail)

Kocha wa Crystal Palace, Roy Hodgson, 72, yuko kwenye mazunguzo kuhusu mkataba mpya. (Sky Sports)

Wolves wanamtolea macho mchezaji wa nafasi ya ulinzi Gabriel Magalhaes wakati huu wakiwa na nia ya kumtafuta mchezaji wa nafasi ya ulinzi mbadala wa machezaji aliyejeruhiwa Willy Boly.(Daily Mail)

Wakala wa mchezaji winga Tahith Chong amewaonya Manchester United kuwa watatazama maombi kutoka sehemu nyingine kama klabu haitawasilisha masharti ya mikataba ya kuridhisha, baada ya mkataba wake kuisha majira ya joto yajayo.(Manchester Evening News)

Chris SmallingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Roma wako tayari kutoa ofa ya pauni 12.9 kwa Manchester United kwa Chris Smalling, 29 baada ya mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi kuanza vyema katika klabu inayocheza ligi ya Serie A. (Guardian)

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 22, huenda akawa amepata jeraha la mguu wakati akishangilia bao lake lililotokana na mpira wa adhabu dhidi ya Chelsea katika michuano ya kombe la EFL.(Mail)

Liverpool imetakiwa kumshawishi nyota wa Chelsea N’Golo Kante,28. (Racing Post, via Mirror)

Newcastle United itafanya mkutano kuhusu usajili wa mchezaji juma lijalo. (Newcastle Chronicle)

Meneja wa Derby County Phillip Cocu amethibitisha kuwa mchezaji wa timu ya taifa ya England Wayne Rooney,34, amekuwa kwenye viwanja vya mazoezi vya klabu hiyo. (Derby County)

Zlatan IbrahimovicHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Vilabu vitatu vinataka kumsajili kiungo wa pembeni wa Juventus Emre Can, 25, katika msimu wa dirisha la usajili mwezi Januari.(Calciomercato)

Meneja wa Saint Etienne Claude Puel amekosoa uamuzi wa klabu kumuuza mchezaji wa nafasi ya ulinzi William Saliba,18, kwenda Arsenal, akisema mpango huo ni wa ”muda mfupi” . (Metro)

Wakala wa Sassuolo , Stefano Sensi amekuwepo Barcelona, na kumfanya kuhusishwa na tetesi kuwa mchezaji huyo atajiunga na mabingwa wa Uhispania. mchezaji huyo anaichezea Inter Milan kwa mkopo. (Sport – in Spanish)

Nantes inataka kumsajili mchezaji wa zamani wa Newcastle Hatem Ben Arfa. Mchezaji huyo wa miaka 32 yupo kwa uhamisho wa bure. (RMC Sport – in French)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW