Michezo

Tetesi za usajili ulaya: Wenger kuvunja kibubu

Kinachofanywa na Ac Milan sokoni kwa sasa hakika ni fujo, inasemekana klabu hiyo ya nchini Italia sasa imehamishia majeshi yake kwa Alvaro Morata na wako tayari kuwapa Real Madrid £70 ili kumnunua.

Golikipa wa zamani wa klabu ya Manchester City Joe Hart anakaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda West Ham na ripoti zinasema hii leo Hart atafanyiwa vipimo vya afya tayari kujiunga na wagonga nyundo hao.

Katika kuonesha kwamba siku zake Chelsea zinakaribia kuisha, Diego Costa ameonekana akila raha kijijini kwao Brazil huku akiwa amevaa jezi ya timu yake ya zamani ya Atletico Madrid.

Manchester United wanakaribia kumsaini winga wa klabu ya Inter Millan Ivan Perisic ambapo inasemekana usajili wa winga huyo unaweza kukamilika mwishoni mwa wiki hii.

Baada ya Ross Barkley kutoswa katika safari ya Everton kuja Bongo sasa kiungo huyo yuko mbioni kuhamia Tottenham ambapo taarifa zinadai kwamba klabu ya Tottenham iko tayari kutuma ofa nono ili kumpata.

Kocha wa Arsenal anaonekana amedhamiria kufanya makubwa ambapo sasa yuko mbioni kutuma ofa mbili kumnunua mlinzi Virgil Van Dijik na mshambuliaji wa Celtic Moussa Dembele.

Ukiachana na usajili wa Dijik na Dembele inasemekana Arsenal wanakaribia kumnunua mlinzi wa Monaco Thomas Lemar ambaye thamani yake inatajwa kuwa £45m.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents