Tetesi za Usajili: Yanga kumshusha Patrick Aussems ‘Uchebe’ ?

Mara baada ya Mnyama Simba kumsajili na kumtambulisha rasmi, Bernard Morrison akitokea Yanga nikama vile Wananchi wamechokozwa maana baada ya masaa 24 tu kupita ghafla Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Senzo Mazingisa akatangaza kujiuzulu.

Lakini kama hiyo haitoshi hazikupita hata dakika zikazuka taarifa kuwa mtu huyo aliyekuwa muhimu ndani ya Simba na kama angekuwa mchezaji basi angekuwa kiungo mchezeshaji kwa namna alivyo bobea na kuwa muhimu pale Kariakoo lakini ikaonekana picha akisaini katika timu ya Wananchi licha ya kuwa mpaka sasa upande wa Jangwani umekaa kimya bila kuongea chochote.

Tetesi zilizopo kwa hivi sasa Yanga wanamrejesha aliyekuwa kocha wa Simba, Patrick Aussems ‘Uchebe’ huku wakitishia tishia kumng’oa Clatous Chama.

Katika tetesi zilizopo ambazo zinazungumzwa kwenye dirisha hili la usajili ni pamoja na Deo Kanda inadaiwa huwenda akatangazwa kwa Wananchi na kilichopo ni swala la muda.

Papy Kabamba Tshimbi inadaiwa anaelekea kwa Mabingwa wa Nchi, Mnyama Simba.

Hizi ni tetesi tu, katika dirisha hili la usajili linaloendelea hapa nchini, ukweli wa yote utajulika tu.

IMEANDIKWA NA HAMZA FUMO, INSTAGRAM @fumo255

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW