Michezo

Tetesi za Usajili: Yanga wanasa kifaa kipya, TP Mazembe watua nchini kimya kimya kuwana Fei Toto, Kelvin John ‘Mbappe’ na Mohamed Hussein, KMC mambo shwari

Ikiwa ligi mbalimbali zimemalizika kwa sasa duniani kote, kinachuzungumzwa katika vinywa vya wapenda soka ni tetesi za usajili kwa baadhi ya timu kuwasajili wachezaji wapya na kuongeza kandarasi kwa wale wazamani ambao muda wao unakaribia kumalizika.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Tv1 Tanzani, viongozi wa TP Mazembe wapo jijini Dar es Salaam wakitafuta saini za wachezaji watatu kutoka Tanzania ambao ni Mohamed Hussein (Simba), Feisal Salum (Fei Toto-Yanga) na kinda Kelvin John ‘Mbappe’. Klabu hiyo ya DRC imetoa ofa ya kumsomesha Kelvin ambaye bado hajafikisha miaka 18.

https://www.instagram.com/p/BzAefJWHBsG/

Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania Bara YangaSC wamekamilisha usajili wa kiungo Mapinduzi Balama kutoka klabu ya alliancefootballclub2011 ya Mwanza kwa mkataba wa miaka mitatu.

https://www.instagram.com/p/BzAn6GHgwVO/

Kupitia akaunti yao ya Instagram, Simba hapo jana ilitangaza kukamilisha usajili wa Mbrazili mwenye umri wa miaka 23, Wilker Henrique da Silva kwa mtaba wa miaka miwili.

https://www.instagram.com/p/By97kpgHxqL/

Nahodha wa klabu ya KMC, Juma Kaseja ameongeza mkataba wa miaka mitatu hadi mwaka 2022 kuendelea kuichezea timu hiyo.

Kupitia akaunti yao KMC wameanika wazi mkataba huo ambao utamfanya Juma Kaseja anaendelea kusalia kwa miaka mitatu zaidi baada ya leo kusaini kandarasi hiyo.

https://www.instagram.com/p/BzAUMMhAL_f/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents