Habari

TFDA: Dawa zilizopo sokoni zina ubora wa asilimia 98

Serikali imewahakikishia wananchi kuwa, dawa zilizopo katika soko zina ubora kwa asilimia 98 na itahakiksha zinaendelea kukidhi vigezo vya ubora kama zilivyokuwa wakati zinasajiliwa kwa mujibu wa sheria, kanuni,miongozo na taratibu za udhibiti.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kueleza mikakati ya Mamlaka hiyo.

“Katika maabara ya TFDA inayokidhi ithibati ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kati ya sampuli za dawa 199 za Binadamu zilizochunguzwa,sampuli 184 sawa na asilimia 92.5 zilikidhi vigezo vya ubora na sampuli za dawa 10 aina ya Ergometrine ya sindano ambayo ni sampuli 5 sawa na asilimia 2.5 hazikufikia ubora kwa kuwa na kiasi cha kiambata hai chini ya kiwango kinachokubalika.”Alisisitiza Sillo

Akifafanua, Sillo amesema kabla ya dawa kusajiliwa na TFDA na hatimaye kuruhusiwa kuingia katika Soko,zinafanyiwa tathmini ya Ubora,Usalama na ufanisi sanjari na ukaguzi wa mifumo ya utengenezaji bora Kiwandani na hizo ni hatua za awali za mifumo ya udhibiti wa dawa duniani.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents