Michezo

TFF imeshindwa mbinu za Cape Verde?

Rais wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli ameanza kazi yake ya kuiongoza Tanzania kwa kasi ya juu na kupasua majipu yalioshindikana.

images

Nakumbuka kilichotokea Oct 11, 2008 pale uwanja wa taifa, Taifa stars ilishinda magoli matatu kwa moja dhidi ya Cape Verde. Magoli ya Stars yalifungwa na Iddy, Tegete na Ngassa huku goli la kufutia machozi la Cape Verde likifungwa na Jose Semedo.

Kipindi timu hizi zinakutana Taifa Stars ilikuwa kwenye kiwango kizuri sana, ikiwa chini ya kocha mbrazil Marcio Maximo ambaye aliwafanya mashabiki kuanza kuipenda timu yao ya taifa. Ni kweli zama zimebadilika ni miaka minane tu imepita lakini hali ilizidi kuwa mbaya kwa timu yetu ya taifa, je ni laana ya Maximo?

Mwaka 2008 Cape Verde ilikuwa inashika nafasi ya 32 kwa Afrika kwenye viwango vya fifa, lakini pia ilikuwa nafasi ya 110 duniani, wakati huo Tanzania ilikuwa inashika nafasi ya 29 kwa Afrika na 101 duniani.

Mwaka 2016 umebadilika ghafla na kuwa mzuri zaidi kwa timu ya taifa ya Cape Verde baada ya Fifa kutangaza viwango vipya vya mpira wa miguu duniani, timu hiyo imeshika nafasi ya kwanza kwa kwa Afrika na pia imeshika nafasi ya 32 duniani. Miaka minane baadaye Tanzania inashika nafasi ya 126.

caboverdefutebol2013b-1

Ubabaishaji wa soka la Tanzania ndiyo huu ambao umeweza kulifikisha soka letu hapa, iko wapi timu ya vijana ya Copa Cocacola iliyoenda Brazil? Wako wapi vijana waliochukua kombe la dunia kwa vijana wanaoishi kwenye mazingira magumu? Tangu yameanzishwa mashindano ya Uhai Cup yamesaidiaje timu yetu ya taifa?

Tumeshindwa wapi kuiga mfano wa timu ya taifa ya Cape Verde ambao walianza kama mchicha lakini kwa sasa wanaonekana kuwa mbuyu, wameshiriki hadi michuano ya kombe la Afrika na kufika nafasi nzuri, lakini sisi tumebarikiwa kufukuza makocha kila siku kuanzia kwenye timu ya taifa na vilabu navyo vimezidi kufuata nyayo kama hizo za kufukuza makocha. Hatuhitaji kuangalia tulipoangukia tunapaswa kuangalia tulipojikwaa kwanza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents