Michezo

TFF, KTA wamezindua programu ya maendeleo ya soka kwa Wanawake

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kwa kushirikiana na Taasisi binafasi ya Karibu Tanzania Association (KTA) kwa pamoja wamezindua programu ya maendeleo ya soka kwa wanawake vijana ili kuhamasisha usawa wa kijinsia, uwezeshaji kijamii na kiuchumi kwa wanawake nchini itakayofadhiliwa na Shirika la Forum Syd kutoka nchini Sweden.

TFF1

Programu hiyo inafadhiliwa na Shirika la Forum Syd la nchini Sweden imewekwa saini na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mia Mjengwa Bergdahl, Mratibu wa Programu hiyo kutoka taasisi ya Karibu Tanzania katika ofisi za TFF zilizopo Karume.

Awali akizungumza Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Jamali Malinzi alisema programu hiyo ni ya aina yake kwani haijawahi kufanyika nchini na inalenga kujenga mfumo utakaotumiwa nchi nzima katika kutoa mafunzo kwa soka la wanawake kwenye maeneo ya ufundi yaani makocha, waamuzi, uongozi na tiba kwenye michezo.

“Programu hii itasaidia kuendeleza vipaji kwa wachezaji wanawake na kuongeza hali ya kujitambua na kujiamini kwa walengwa na lengo ni kuongeza idadi ya wachezaji wenye ubora na viwango kwa soka la wanawake katika ngazi zote hivyo programu hii ni nyenzo ya kuwawezesha wanawake,” alisema Malinzi.
Kozi hii itakuwa inafundishwa katika vyuo 55 vya Maendeleo ya Jamii na kwa kuanzia kozi 20 zitafundishwa katika vyuo 20 kwenye kanda saba.
Jumla ya wanawake 600 ikiwamo 30 kutoka katika kila vyuo vya Maendeleo ya Jamii watashiriki.
Katika programu hii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wanashiriki kikamilifu kwa kuwezesha wanafunzi na miundo mbinu ilivyo chini ya wizara hiyo kutumika katika kufanikisha programu hii.
Mafunzo yatatolewa sambamba na mafunzo mengine ya kawaida yanayotolewa kwenye Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi, kama vile maarifa ya jumla na mafunzo ya ufundi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents