Michezo

TFF kukutana na vyuo soka la ufukweni

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), leo Novemba 10, 2017 linakutana na viongozi wa vyuo kuzungumza taratibu zitakazotumika kwenye ligi ya soka la ufukweni itakayoanza Novemba 18, mpaka Desemba 9, mwaka huu kwenye Ufukwe wa Escape One, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kitajadili usajili wa wachezaji, taratibu mbalimbali zitakazotumika pamoja na kupokea maoni ya vyuo hivyo.

Kikao hicho kitafuatiwa na mafunzo kwa vyuo vyote shiriki yatakayofanyika Novemba 13, mwaka huu.

Mpaka sasa vyuo mbalimbali tayari vimethibitisha kimaandishi kushiriki kwenye mafunzo hayo.

Vyuo vilivyothibitisha kushiriki ni Chuo cha Ardhi, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Chuo Cha Ufundi (DIT), Chuo cha Usafirishaji (NIT), Chuo cha Elimu ya Tiba cha Kahiruki, Chuo cha Elimu ya Biashara cha Lisbon, Chuo cha Silva , Chuo UAUT, TIA, El-Maktoum collage jjEngineering, Magogoni, Chuo cha uandishi wa habari DSJ na TSJ.

Wakati huo huo kozi ya waamuzi wa Soka la Ufukweni iliyoanza Novemba 7, 2017 katika Makao Makuu ya TFF Karume, Dar es Salaam inamalizika kesho Jumamosi Novemba 11, 2017.

Waamuzi hao wanaohitimu watashiriki katika mashindano ya vyuo yatakayoanza Novemba 18.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents