Michezo

TFF kununua madawati fedha zitakazopatikana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii

Shirikisho la soka nchini (TFF) limetangaza kuwa fedha zitakazopatikana kwenye mechi ya Ngao ya Jamii zitatumika kuchangia kwenye ununuzi wa madawati kwa shule ambazo zina uhaba huo.

TFF

Mchezo huo unaotarajiwa kufanyika leo kwa kuzikutanisha timu mbili za jiji moja kati ya Yanga dhidi ya Azam FC kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya ligi kuu Tanzania Bara kuanza hivi karibuni.

Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema, “TFF haijalenga kupata mapato ya kesho “kwenye Ngao ya Jamii kwaajili ya mpango wowote wa maendeleo ya shirikisho.”

“Tumelenga kuisaidia na kuipa support serikali katika mpango wake wa kusambaza madawati kwa shule za msingi ili wanafunzi wasikae tena chini. Kwa upande wetu TFF tunatoa madawati 200,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents