Michezo

TFF watoa pongezi kwa Tenga

Shirikisho la Soka nchini Tanzania TFF  kupitia kwa Kaimu Rais wake, Wallace John Karia limempongeza Leodegar Chilla Tenga ‘Rais wa Heshima wa TFF ‘ kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Kamati ya Ufundi na Maendeleo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Picha inayohusiana
Leodegar Chilla Tenga

Leodegar Chilla Tenga aliteuliwa Ijumaa hii katika Mkutano Mkuu wa CAF uliofanyika mjini Rabat nchini Morocco ambako katika kamati hiyo muhimu, Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zambia (FAZ), Kalusha Bwalya naye aliteuliwa.

Hii ni sifa kwa nchi. Na ni sifa kwa Mheshimiwa Tenga. Tunajisikia fahari Tanzania kung’ara katika medani za uteuzi katika vyombo vya kimataifa kama CAF. Uteuzi wake ni kwamba anafungua njia kwa nchi na wengine ili kufanya vema,” amesema Karia.

Karia amesema ana imani na Tenga na Bwalya katika kamati yao kwa sababu ni wachezaji na manahodha wa zamani wa timu za taifa. Itakumbukwa kwamba Tenga alikuwa akicheza kama mlinzi kwenye timu ya Taifa ya Tanzania na Bwalya alikuwa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Zambia.

Katika mkutano huo mbali na kuteua akina Tenga na kuunda kamati nyingine, pia ulifanya marekebisho ya muundo wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) na sasa yatakuwa yakifanyika katikati ya mwaka badala ya mwanzoni mwa mwaka.

Mbali namarekebisho hayo ya AFCON, pia idadi ya timu za kushiriki zimeongezwa kutoka 16 hadi 24 hii yote ili kuongeza ushindani.

Watanzania wasikate tamaa, hata kama kwa mfumo wa sasa unaofutwa au tuseme kubadilishwa, bado tuna malengo yetu yalikuwa ni kufuzu, Tunajipanga kwa hali ya sasa na hatujaanza vibaya na Lesotho bado tuna nafasi,” amesema Karia.

Mabadiliko hayo ya AFCON yataanza kutumika kuanzia kuanzia Fainali za mwaka 2019 nchini Cameroon .

Hii si mara ya kwanza kwa Tenga aliyepata kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), bali amekuwa akiteuliwa mara kwa mara kuwa Mjumbe wa Kamati mbalimbali za CAF.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents