Michezo

TFF yaanza kuuza tiketi za Fainali kombe la Dunia 2018

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea tiketi 290 kutoka kwa Shirikisho la Kimataifa la soka (FIFA) kwa Watanzania watakaotaka kwenda kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Russia mwakani 2018.

Tiketi hizo zipo kwenye makundi mbalimbali yaliyogawanywa kulingana na aina ya mechi na hatua mbalimbali za mashindano hayo ikiwemo hatua ya makundi na zile zinazofuata.

TFF inalo jukumu la kusimamia zoezi hilo la uuzwaji wa tiketi hizo kwa Tanzania ambapo mwisho wa zoezi hilo ni Januari 15, 2018. Kwa yeyote mwenye nia ya kununua tiketi awasiliane na Idara ya mashindano TFF.

Wakati huohuo, utaratibu wa kadi maalumu za kuingilia Uwanjani kwa waandishi wa habari kutoka Tanzania (accreditation) katika mashindano hayo ya Kombe la Dunia Russia uko tayari na waandishi wanatakiwa kujaza kupitia link maalumu inayosimamiwa na Idara ya habari na mawasiliano ya TFF.

Kwa mwana habari yeyote anayetaka kuripoti fainali hizo za kombe la Dunia awasiliane na Idara ya Habari na Mawasiliano TFF ili aweze kuthibitishwa FIFA ambapo mwisho wa zoezi hili ni Januari 15, 2018.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents