Michezo

TFF yadai ni klabu mbili tu zilizokamilisha usajili

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezikumbusha klabu zote ambazo zinasimamiwa na Shirikisho hilo kuhakikisha zinamaliza zoezi lake la usajili mapema.

Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Kwa mara nyingine, tunazikumbusha klabu 16 za Ligi Kuu ya Vodacom, 24 za Ligi Daraja la Kwanza na 24 Ligi Daraja la Pili kusajili wachezaji haraka kwani zimebaki siku 11 tu kabla dirisha halijafungwa.

Hadi sasa ni timu mbili, kati ya 62 ndizo zimesajili huku TFF ikisemakuwa haitaongeza siku kama ilivyofanya kwa mwaka jana.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza kufungua dirisha la usajili kwa wachezaji wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili ikiwa ni ufunguzi wa msimu mpya wa mashindano wa 2017/2018.

Mpaka sasa klabu mbali mbali zinaendelea na usajili katika kwa ajili ya msimu mpya wa ligi huku Singida United ikiwa imekamilisha usajili wake kwa kumpa mkataba wa miaka miwili winga wa Ndanda FC, Kigi Makasi aliyehudumu kwa nyakati tofauti timu ya Taifa ya Tanzania, Simba S.C na baadae Ndanda Fc.

Dirisha la usajili lilifunguliwa Juni 15, mwaka huu na litarajia kufungwa Agosti 6, mwaka huu.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents