Michezo

TFF yataja viingilio vya Azam FC vs Simba SC

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ‘TFF’ limetaja viingilio vya mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara baina ya timu ya Simba SC dhidi ya Azam FC mchezo utakao chezwa katika dimba la Azam Complex Septemba 9 mwaka huu.

Katika duru la kwanza la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania ‘VPL’ Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, ilianza na ushindi mwembamba baada ya kuichapa NdandaFC  bao 1-0, katika mtanange uliyochezwa katika dimba la Nangwanda Sijaona.

Wakati Simba SC wao wakianza msimu vyema baada ya kuichapa mabao 7-0 Ruvu Shooting huku mchezaji wao raia wa Uganda, Emmanuel Arnold Okwi akifunga manne kati ya hayo.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents