Michezo

TFF yatangaza mabadiliko ya Katiba, nafasi ya Makamu wa Rais sasa ni ya kuteuliwa, idadi ya wajumbe kupunguzwa

Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao ameweka wazi mabadiliko ya Katiba ya shirikisho hilo ambayo kwa kiasi kikubwa yanahusu mfumo wa uongozi kuelekea uchaguzi ujao.

Moja kati ya mambo yaliyoguswa ni nafasi ya Makamu wa Rais ambapo kuanzia sasa hatachaguliwa kwa kupigiwa kura bali atakuwa akiteuliwa na Rais.

Mabadiliko mengine yamegusa idadi ya wajumbe wa kamati ya utendaji ambayo sasa itapungua kutoka 22 hadi 13, huku kanda nazo zikipunguzwa kutoka 13 hadi 6.

Vilevile katika mabadiliko hayo wajumbe wa mkutano mkuu watapungua kutoka 129 hadi 87, ikimaanisha kuwa kila mkoa katika mikoa 26 ya Tanzania Bara utatoa wajumbe wawili, wajumbe 20 watatoka kwenye vilabu huku vyama washirika wakitoa wajumbe 15.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents