Michezo

TFF Yatoa Onyo Yanga

 

Shirikisho la soka Tanzania ,TFF, kimeionya timu ya soka ya Yanga,iwapo itashindwa kuwalipa wachezaji wake wanaodai fedha za kukatishwa mikataba yao,Wisdom Ndlovu ‘Stephen Malashi’ na ‘John Njoroge’ ,litalazimika kuingilia kati sakata hilo.


Ofisa habari wa TFF Florian Kaijage amesema swala hilo limeshafikishwa katika ofisi za shirikisho na iwapo klabu hiyo ya jangwani itaendelea kuyapuuzia madai hayo,itachukuliwa hatua na kamati ya maadili.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Yanga ilisema itawalipa wachezaji hao hivi karibuni. Mapema wiki hii TFF imesema kama klabu hiyo itaendelea kuwazungusha wachezaji basi watachukua uamuzi kwa mujibu wa kanuni zao.

‘Ni kweli swala hilo limetufikia na tumepanga kuingilia kati kama klabu hiyo [YANGA]itaendelea kuchelewa.Kimsingi tumepanga kulipeleka suala hilo kwenye kamati ya maadili na utawala wa wachezaji ambao ndio wanahusika kwenye migogoro huo. Tunaipa klabu ya Yanga  muda kabla hatujachukua hatua zetu kama shirikisho.Tutawataarifu hatua tutakazochukua kama Yanga wataendelea kuwasumbua wachezaji hao’ alisema Kaijage.

Kwa upande mwingine katibu mkuu wa Yanga Lawrende Mwalusako alipoulizwa juu ya hilo suala alisema hawezi kulizungumzia.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents