Michezo

TFF yatoa ufafanuzi uhalali wa dakika 120 za Singida United Vs JKT Tanzania

Baada kutokea sintofahamu kwenye mchezo wa nusu fainali Kombe la  Shirikisho  la  Azam  (Azam Sports Federation Cup – ASFC), kwa kuongezwa dakika 30 kwenye mchezo uliyowakutanisha Singida United dhidi ya JKT Tanzania na kumalizika kwa 2 -1, hatimae TFF imetolea ufafanuzi swala hilo.

Kufuatia minong’ono na malalamiko ya hapa na pale kwa baadhi ya wapenzi wa soka kutaka kufahamu kanuni zilizotumika kuamuru kupigwa dakika 30 za nyongeza badala ya hatua ya mikwaju ya penati kama wengi walivyotarajia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema kuwa kwa mujibu wa kanuni ya nane ya mashindano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) za mwaka 2017 inazungumzia mshindi anavyopatikana.

 

Klabu ya Singida United imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup – ASFC), baada ya kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania kwenye dimba la Namfua mjini Singida baada ya mchezo huo kufika hadi dakika 120.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents