Michezo

TFF yawaondoa wachezaji wa Simba ndani ya ‘Taifa Stars’, viongozi wao kupelekwa kwa pilato

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limewaengua katika kikosi cha timu ya taifa ‘Taifa Stars’ wachezaji sita wa timu ya Simba kutokana na kuchelewa kuripoti kambini kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na kocha, Emmanuel Amunike.

Katibu mkuu wa TFF, Wilfred Kidao

Nyota hao walitakiwa kuripoti kambini jana usiku huku wakiwa wamepewa taarifa wakati Aishi Manula pekee ndiye aliyeripoti.

Katibu mkuu wa TFF, Wilfred Kidao amewaambia waandishi wa habari kuwa kocha Amunike amekasirishwa na kitendo hicho na kuamua kuchukua maamuzi hayo amabayo Shirikisho hilo chini ya Rais Wallace Karia wamelipitisha.

“Wachezaji wote wa Simba walioitwa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ isipokuwa Aishi Manula wameenguliwa katika kikosi kinachojiandaa na mchezo wa kufuzu dhidi ya Uganda kutokana na kutoripoti kambini kwa muda uliopangwa,” Wilfred Kidao Katibu Mkuu TFF.

Kidao ameongeza kuwa TFF iliamua kusogeza mbele mechi za Simba, Azam na Yanga zilipokuwa zichezwe Septemba mosi na pili ili kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za Afrika dhidi ya Uganda ‘The Cranes’ utakaofanyika Septemba 8 jijini Kampala. “TFF imewaengua wachezaji sita wa Simba kwenye kikosi cha timu ya taifa kutokana na kuchelewa kuripoti kambini licha ya kupewa taarifa mapema,” alisema Kidao.

Wachezaji hao ni Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, John Bocco na Shiza Kichuya.

Mbali na wachezaji hao viongozi wa Simba, Hamisi Kisiwa na meneja Richard Robert watapelekwa katika kamati ya maadili ya TFF siku ya Jumamosi ili kuchukuliwa hatua.

Related Articles

13 Comments

  1. watovu Wa Nidhamu Na simba Ipo kwenye Ubora sana Na kutokana a Hilo wachezaji Wao wameanza kujisikia Mbona aishi manula yeye Kazingatia maagizo ya Mwalimu Mnakosa Baraka kwa watz kisa Huo usimba na Uyanga Kuweni Wazalendo Lakini sio mbaya kuna vijana pia wameitwa mlipotoka Nyie Acha waonesha cheche..

  2. 5-0 mbn chache huyu Amonike anadhani Uganda niwakuchezea program yamaandali ilitakiwa kwa pamoja mechi trh 12 mchezaji kachelewa Siku moja unamuondoa wayanga nawaliopo nje hawajafika hiyo program unatengeneza kwa timu nusu angekuwa nasubra timu ikamilike kilalaheri Uganda na safari ya kocha kubakia Tanzania nindogo kama kaanza kwa mbwembwe

  3. Kocha kafanya cha maana sana kuwaondoa wakina simba maana simba wanajiona wenyewe ndo Tanzania kabsa hawajui kuwa ni nafas pekee wanayo kuwa wamependelewa kutoka ktk vilabu vitatu simba ,,,,yanga na azam ambapo kuna vilabu vingne vina tamani wachezaji wao kuwemo kwenye timu ya taifa na havimo mm naona tuna vilabu vingi sana hapa bonge hebu wapewe nafasi na vilabu vingne waonyeshe uwezo wao na wanaweza fanya vzr zaid ya hao wanaolinga linga

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents