Habari

Thabo Mbeki awachochea wabunge wa ANC

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki amewataka wabunge kutoka chama cha ANC kuangalia kinachoendelea katika nchi hiyo kwa maslahi ya wananchi na siyo kwa ajili ya kukilinda chama pekee.

Wiki ijayo bunge la nchi hiyo litajadili muswada wa kutokuwa na imani na rais Jacob Zuma ambaye ametakiwa kujiuzulu kwenye kiti hicho kutokana na ufisadi unaodaiwa kutokea kwenye chama cha tawala.

Mbeki amewataka wabunge wote kuwa sauti ya wananchi na wala sio sauti ya vyama vyao vya kisiasa. Rais huyo mstaafu alijiondoa kwenye chama hicho Septemba 20 ya mwaka 2008 ikiwa ni miezi tisa tangu alipotoka kwenye nafasi yake ya urais.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents