Michezo

Thailand ya dhamini kombe la EFL Cup ya Uingereza

Michunao ya kombe la EFL cup  ya nchini Uingereza  sasa itajulika kama Carabao Cup kutokana na kupata udhamini mpya wa kampuni ya Carabao ya nchini Thailand

Kampuni hiyo inayotengeneza Kinywaji cha kuongeza nguvu mwilini imesaini mkataba wa miaka mitatu wa kudhamini michuno hiyo.

Ratiba ya kupanga droo ya mechi za raundi ya kwanza ya michuano hiyo itafanyika ijumaa hii huko Bangkok, Thailand.

Michezo ya kwanza itafanyika kati ya Agosti 8 na 9 na mchezo wa fainali utapigwa katika dimba la Wembley Februari 25, 2018.


Klabu ya Manchester United ndio bingwa mtetezi wa michuano hiyo.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents