Burudani

The Game awataka Breezy na Drake kuyamaliza kiutuuzima


Rapper wa West Coast The Game ametoa maoni yake kuhusiana na ugomvi kati ya Chris Brown na Drake uliotokea hivi karibu kwenye club ya usiku na kudai kuwa wasanii hao wanapaswa kusuluhisha ugomvi huo haraka.
Rapper huyo ambaye amewahi kuwashirikisha wasanii hao wote amesema wanatakiwa kuepuka shari itawale uhusiano wao.
Akiongea na TMZ, The Game amewataka wasanii hao kuweka uadui wao pembeni, “Chris Brown ni kama mdogo wangu, …Drake ni mshkaji poa. Wanahitaji kupotezea, haina faida,” alisema.
The Game, ambaye si mgeni katika beef kama hizi, aliongeza kuwa hana haraka ya kutaka kuwasuluhisha marafiki zake hao wawili.
“I’m gonna stay out of their beef … it’s for the birds,” alisema.
Katika hatua nyingine Chris Brown amevishambulia vyombo vya habari kwa kuita uandikwaji wa habari hiyo kama “full of s**t.”
Ripoti za awali zilidai kuwa Brown alipeleka chupa ya pombe kwenye meza ya Drake kama ofa ya kawaida lakini Drake hakufurahia.
Baadaye chupa zilirushwa kwenye klab hiyo ya jijini New York na ndipo timbwili likaanza. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa ugomvi huo umetokana na uhusiano wa wasanii wote hao na mwanadada Rihanna.
Juzi msanii huyo mwenye miaka 23, aliuporomoshea matusi mtandao wa TMZ.
“Tmz y’all full of s**t!!!! It’s insane how your stories are not informative at all and far from f**king facts! (sic)”
“It’s really sad! All y’all in that office sit behind a desk and hide behind ur lives by trying to tarnish others! Good game!”
“The media will always try to slam dunk!!! But I win my games with lay ups! Godbless! ?#knowyourfacts”
“It upsets u that I’m not this hoodlum,enraged,young black man you wanna portray me as. They did it to Mike.. I can handle it! ?#imdone? (sic), aliandika.
Polisi wanachunguza mkanda wa video wa tukio hilo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents