Burudani

The Rock kuwania urais wa Marekani 2020

By  | 

Huenda uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2020 ukawa na mvuto mkubwa kutokana na baadhi ya mastaa kibao wa nchi hiyo kutamani kukalia kiti cha urais.

Muigizaji wa Fast and Furious, Dwayne ‘The Rock’ Johnson huenda akawa ni mmoja kati wa wagombea wa nafasi hiyo. Akifanya mahojiano na GQ, muigizaji huyo ameonekana kuitamani nafasi hiyo ambayo kwa sasa inashikiliwa na Donald Trump.

“Personally, I feel that if I were president, poise would be important. Leadership would be important,” The Rock ameuambia mtandao huo.

“Taking responsibility for everybody. [If I didn’t agree with someone] on something, I wouldn’t shut them out. I would actually include them. The first thing we’d do is we’d come and sit down and we’d talk about it. It’s hard to categorize right now how I think he’s doing, other than to tell you how I would operate, what I would like to see,” ameongeza.

Naye Kanye West alitangaza kuwa atagombea Urais katika uchaguzi ujao, alipozungumza kwenye MTV Video Music Awards August mwaka jana. Tangu hapo, Barack Obama, Donald Trump na Hillary Clinton wote wamewahi kutoa ushauri kwa Yeezy kuhusu azma yake hiyo.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments