Bongo Movie

The Secret of Toy ya Hemed na Flora Mvungi yafanana na filamu nyingine yenye jina na story hiyo hiyo


Kampuni ya usambazaji wa filamu ya Pili Pili Entertainment imejikuta kwenye mtihani mgumu baada ya kununua filamu iitwayo The Secret of Toy iliyowashirikisha waigizaji kama Hemed Suleiman, Flora Mvungi, Saidi Omar na Maryam Said, huku kukiwa na filamu nyingine ya Kiswahili yenye jina na story hiyo hiyo.

Filamu hiyo imefanywa na Momix Video Production, ikiongozwa na Said Omari, na hadithi ikidaiwa kuandikwa na Aisha Ali na kutayarishwa na Ally Mgeni.

Katika Take One ya Clouds TV jana kumeoneshwa vipande vya filamu hizo vinavyofanana kila kitu japo waigizaji ni tofauti.

Katika kipindi hicho alihojiwa mtunzi halisi wa kisa hicho cha The Secret of Toy ambaye anasema ameibiwa wazo lake la filamu ambayo tayari alikuwa ameshaishoot.

“Mimi nilikuwa na story yangu. Nilivyokuwa na story yangu nikamtafuta huyo Taita ambaye alikuwa ni mwalimu wangu wa mazoezi,” alisema Magreth. “Sasa baada ya kumtafuta akawa anaendelea naye kunifundisha mazoezi yaani ya kuigiza. Baadaye nikamwambiaje, ‘mimi nina story’ akaniambia ‘story gani’? nikamwambia ‘Secret of Toy’. Nilipomwambia Secret of Toy akaniambia umeshaiandikia script, nikamwambia hapana akaniambia basi nipe niiandikie script, nikampa. Baada ya muda akamaliza kuandika. Alipomaliza akaniambia tayari nimeshamaliza.”

Aliendelea, “Nikamwambia sasa mimi sina idea vizuri sana na mambo ya sanaa, lakini wewe kama unaweza ukanisupport kwa mambo ambayo siyafahamu mimi nipo radhi nigharamie tuicheze, akasema sawa, kweli tukafanya hivyo, nikamuuliza kuhusu wasanii akaniambia yeye atatafuta wasanii ambao atawapata, ambao hatawapata na mimi nitatafuta. Basi tukafanya hivyo, mwisho wa siku tukapata wasanii, akawaleta wengine nikatafuta mimi, tukaanza kushoot.

Tumeshoot mpaka tumemaliza yaani zikabaki kama scene nne kuisha, zilipobaki scene nne akabadilika akawa ananitaka kimapenzi, mimi nikamwambiaje, tusichanganye mapenzi na kazi, hii ni kazi tufanye kazi ili tuuze mwisho wa siku tupate pesa. Kumbe mwenzangu hakuridhika na hivyo nilivyomweleza. Toka nilipomwambia hivyo siku ya pili yake akaja location maana yeye ndio alikuwa anadirect, tukashoot kama scene mbili akaondoka ghafla, mimi sikujua ameenda wapi. Nilivyowauliza na wasanii wakaniambia kuwa hajaaga, ikabidi tujidirect hivyo hivyo, wasanii wajidirect wenyewe mimi napoelewa naelekeza ambapo sielewi basi.

Baada ya siku mbili nilipomgia simu akapokea akaniambiaje, mimi ndio nimeshika story yako iko mikononi mwangu, halafu nakuambia unaniletea jeuri sasa tuone kama hiyo kazi utaweza kuifanya.”

Magreth alisema baada ya muda alijaribu kumbembeleza muongozaji huyo ili kama anahitaji fedha ampe lakini alikataa. Kazi ya kushoot ilikwama baada ya cameraman wao kuugua kwa muda bila kupata nafuu na hatimaye alifariki.

“Nikawa nimekaa na mimi nikapata matatizo ya hapa na pale, sasa kipindi najipanga labda nimalizie zile scene nne ili niiedit niitoe movie yangu nikapigiwa simu na rafiki yangu niko kazini ananiambia nimeona Secret of Toy imebandikwa matangazo.”

Baada ya kutoamini maneno hayo ndipo aliamua kwenda kuona matangazo hayo na kukuta ni kweli.

“Kweli yaani nilichanganyikiwa na niliumia sana,” alisema Magreth kwa simanzi.

Anasema aliamua kuwasiliana na wasambazaji wa filamu hiyo kuwaataarifu kuhusu mkasa wake ambao walisema filamu hiyo wameinunua kwa ‘Bambucha’ ambaye baada ya kumpigia simu alidai kuwa hilo ni wazo lake na labda ni mgongano tu.

“Yaani kila kitu kinafanana na movie yangu, hakuna hata walichobadilisha hata kimoja.”

Hata hivyo haikulikani ni hatua gani zimechukuliwa ili apate haki yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents