Burudani

The Weeknd atoa onyo kwa Wizkid na wasanii wengine wanaotumia neno ‘StarBoy’

Msanii wa muziki kutoka Canada, The Weeknd amewaonya wasanii wa muziki dunia akiwemo Wizkid kuacha mara moja kutumia neno ‘StarBoy’ kwa madai kuwa neno hilo ameshalilipia (TradeMark) kwa matumizi yake ya kibiashara.

The Weeknd na Wizkid

The Weekend amesema kuwa yeye ndiye muanzilishi wa neno/nembo hiyo ya ‘StarBoy’ na yeyote atakayetumia atachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Tayari wanasheria wa The Weeknd wameshaandaa nyaraka za kuwaburuza Eymun Talasazan mahakamani kwa kutumia nembo hiyo kwenye vipindi vyake vya TV baada ya The Weeknd kuachia album yake ya ‘StarBoy’ mwaka 2016.

Wimbo wa ‘StarBoy’ ni moja ya nyimbo zilizopo kwenye album hiyo na ulifanikiwa kushika namba moja kwenye chati za Billboard top 100.

Kwa The Weeknd wimbo wa StarBoy ni wimbo wa tatu kushika namba moja kwenye chati hizo maarufu zaidi duniani.

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents