Burudani

The Weeknd na ex wake Bella Hadid warudiana tena!

The Weeknd na Bella Hadid wamerudiana? Hilo ndio swali ambalo mashabiki wengi wanajiuliza kwa sasa.

Kwa mujibu wa mtandao wa E! News umeripoti kuwa wawili hao wameonekana wakiwa pamoja huku Jumanne hii The Weeknd akionekana akitoka kwenye nyumba ya Bella huko mjini New York.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu cha wawili hao, kimethibitisha ukaribu wa wawili hao kwa kusema, “They enjoy each other’s company and have a lot of fun together. He has expressed to her that he loves her still, and they will always have a real connection. He also apologized for hurting her in the past.”

Wawili hao waliwahi kuwa na mahusiano kwa muda wa miezi 18 na waliachana mwezi Novemba mwaka jana ambapo The Weeknd alionekana kuwa na mahusiano na Selena Gomez huku Hadid akidaiwa kutoka na Drake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents