Habari

The World’s Billionaires: Bill Gates aongoza, Aliko Dangote aongoza Afrika, Rostam Aziz ndiye Mtanzania pekee kwenye orodha-Forbes

Jarida la Forbes limetoa orodha mpya ya mabilionea wa dunia kwa mwaka huu 2014. Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft amerejea katika nafasi ya kwanza baada ya miaka mine, huku utajiri wake ukikadiriwa kufikia dola bilioni 76 kwa mwaka huu , ukiwa umekuwa kutoka dola bilioni 67 mwaka jana (2013).

bill-gates-600x403
Bill Gates

Mr Gates amemuondoa bilionea wa Mexico Carlos Slim aliyekamata nafasi ya pili katika orodha hiyo mwaka huu, kutoka nafasi ya kwanza aliyoikamata mwaka jana.

Waanzilishi wa Whatsapp pia wamefanikiwa kuingia katika orodha ya mwaka huu baada ya kufanya dili ya dola bilioni 19 na Facebook , Jan Koum akikamata nafasi ya 202 huku mwenzake Brian Acton akikamata nafasi ya 551 .
Aliko-Dangote
Alika Dangote

Bilionea wa Nigeria Aliko Dangote ambaye pia anamiliki kiwanda cha Saruji mjini Mtwara, ameendelea kuwa Mwafrika tajiri zaidi katika orodha hiyo ya Forbes kwa utajiri wa dola bilioni 25.

Rostam
Rostam Aziz

Rostam Aziz ndiye Mtanzania pekee aliyeingia katika orodha ya Forbes ya mabilionea wa dunia kwa mwaka huu, na kushika nafasi ya 1565 akiwa na utajiri wa dola bilioni moja.

Ingia hapa kusoma orodha nzima

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents