Burudani

‘Thriller’ ya Michael Jackson kurudi kwa mfumo wa kisasa

Mnamo Novemba 30, mwaka 1982 dunia ilishuhudia albamu ‘Thriller’ kutoka kwa msanii nguli wa muziki wa Pop duniani Michael Jackson.

Nitakribani miaka 35 tangu msanii huyo aachie albamu hiyo yenye ngoma saba na sasa itaweza kupatikana katika toleo jipya la 3D, litakalotoa nafasi kwa mashabiki wa msanii huyo kufaidi upya muziki wa legendary huyo imebainishwa na muongozaji John Landis.

Albamu hiyo itakuwa katika mfumo wa kisasa wa teknologia na itafanyiwa vionjo mbalimbali vya sauti ili kuleta radha stahiki ya muziki wa pop.

“Michael and I always intended it to be seen in a cinema. When you watch in on YouTube, you don’t see how it is supposed to be. Now you can see the way Michael intended it to be,” amesema Landis.

Akaongeza “My only disappointment is that he is not here to see it because he’d love it!.” Original albamu ya ‘Thriller’ ilitengenezwa chini ya Epic Records pamoja na CBS Records, Michael Jackson alifariki mwaka 2009 akiwa na miaka 50.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents