Burudani

THT kusaka vipaji vipya vya waimbaji kesho

Nyumba ya vipaji Tanzania, THT, imetangaza leo kuwa jumapili ya kesho tarehe 3/3/2013 watafanya usaili wa kusaka vipaji vipya katika ofisi zao za THT Block 41 zilizo karibu na Nyumbani Lounge (Kinondoni).
Usaili huo utaanza saa tano kamili asubuhi, ukihitaji vijana wenye vipaji kuanzia miaka kumi na sita hadi ishirini na nne.
THT inasifika kwa kukuza na kuzalisha vipaji vingi vya kucheza na kuimba hapa nchini, wakiwemo wasanii kama kina Barnaba, Rachel, Linah, Mwasiti, Ali Nipishe, Amini, Ditto, Makomando na wengine wengi.
Akizungumzia usaili huo,meneja masoko wa THT, Michael Nkya, alisema anawakaribisha vijana wenye vipaji kujiunga THT.
‘THT ni sehemu ya kila kijana mwenye kipaji, hivyo usisite kuja, kama una kipaji njoo, nasi tutakuchagua kwani hakuna upendeleo wowote’ alisisitiza Nkya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents