Burudani

TID amshutumu promota wa UK kuwa kamwacha ‘solemba’ bila kumlipa, apanga kumpigia balozi

Ni majanga kwa kwenda mbele kwa Top in Dar. Staa huyo aliyepiga show ya nguvu weekend hii jijini London, Uingereza ameibuka na kusema kuwa promota wa show hiyo, Victor aka Dj Rule amemuacha kwenye mataa baada ya show. TID alitumbuiza pamoja na Jaguar wa Kenya.

Kupitia Facebook, TID ambaye jina lake halisi ni Khalid Mohamed ameandika:

“My mind is not some stupid promota is trying to rob me,am not goin to let it happen am calling my balozi why a Kenyan artist hajamzingua……ndo maana hatuendelei. DJ rule victor amekimbia hela zangu hajanipa left me in a hotel hang in like a fan.”

Jitihada za kumtafuta Dj Rule azungumzie suala hili zimegonga mwamba kutokana na kutopokea simu yake.

165870_368390846590053_1361863796_n
Dj Rule

Hata hivyo Dj Victor aliandika kuwa show hiyo ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa na kumpongeza TID kwa kwenda kwenye show siku chache tu baada ya kumzika Mangwea.

“The East African Superstars at the sold out TID & Jaguar last night at the Ville London thanxs mostly to TID who made it at last after his dear friend passing on few days ago.”

Kwa upande mwingine mambo si mabaya kwa Jaguar baada ya show hiyo kwakuwa alitweet picha hii yenye ujumbe, “……thanx London..off to 254.”

BMV4ZqHCQAEOQBA

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents