TID Apewa Siku 10

Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayetumikia kifungo cha mwaka mmoja jela, TID ametakiwa kutoa taarifa ya kusudio la kukata rufaa katika Mahakama Kuu. TID anatakiwa kutoa taarifa za kusudio lake hilo ndani ya siku 10 kuanzia jana

TID Apewa Siku 10

 

Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayetumikia kifungo cha mwaka mmoja jela, Muhamed Khalid ‘TID’ ametakiwa kutoa taarifa ya kusudio la kukata rufaa katika Mahakama Kuu. Akitoa maelezo hayo jana, Dar es Salaam, Jaji wa Mahakama Kuu, Robert Makalamba alisema TID anatakiwa kutoa taarifa za kusudio lake hilo ndani ya siku 10 kuanzia jana na alimpa siku 45 kuandika ombi la kukata rufaa.

Muda wa awali aliotakiwa kukata rufaa wa siku kumi baada ya siku ya hukumu umepita. Lakini, wakili wa msanii huyo Masako Thomas, alisema kuwa Hakimu aliyemhukumu TID hakumweleza mteja wake kama alikuwa anaweza kukata rufaa ndani ya siku 10. Thomas aliwaambia waandishi wa habari nje ya mahakama hiyo, kuwa hakimu huyo alikiuka sheria, kwa kuwa kisheria alitakiwa kumweleza hayo yote msanii huyo.

Katika hatua nyingine, kuliibuka mtafaruku kati ya baadhi ya wanahabari na kijana mmoja aliyekuwa akiwazuia kuingia ndani ya chumba ambacho kesi ilikuwa ikiendelea. Hata hivyo, ndugu wa karibu wa TID waliokuwapo mahakamani hapo waliwaambia waandishi kuwa hawana uhusiano na kijana huyo na pengine ni shabiki. Jaji Makalamba aliamuru TID arudishwe gerezani mpaka taratibu za rufani zitakapokamilika.

TID aliongozwa na maaskari kurudishwa gerezani ambapo akiwa njiani kurudi katika chumba cha mahabusu alisalimiana na mama yake mzazi na ndugu zake waliokuwa wamekaa nje wakisubiri yatakayojiri katika chuma cha mahakama. Julai 23 mwaka huu, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kinondoni, Hamisa Kalombola alimhukumu kijana huyo kwenda jela mwaka mmoja kufuatia kuridhika na mashahidi wote wanne na ushahidi walioutoa mahakamani kuwa TID alimpiga kichwani na mkononi kijana aliyefahamika kwa jina la Ben Mashibe.

Source: Habari Leo

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents