Burudani

TID: Bongo Flava music is so stupid!!!

543738_10150906157803749_1850143035_n

Inaonekana bado mambo hayamwendei poa Top In Dar licha ya kuwa na hit ya ‘Kiuno’ hewani ambayo imeendelea kufanya poa.Hiyo ni baada ya nyota huyo ambaye jina lake halisi ni Khalid, kuamua kutumia Facebook kutoa maoni yake jinsi muziki huo unavyoenda.

“This Bongo Fleva Music is so stupid yaani kiasi kwamba we don’t even sell it only adios get sponsorship to play it lakini sisi tuko majalala,” aliandika TID.

Ujumbe huo ulivuta hisia za Chidi Benz ambaye aliamua kuchangia kwa kuandika: Uoga. Unazaa vijana wanataka ustaa so wanakubali chochote. Wakongwe wanataka maisha so wanahitaji kuongezwa chochote. Vitu vinagongana vitu havieleweki.

Chidi aliongeza,”Watangazaji na wadau wamekua mameneja. Haikatazwi. Ila kama wewe si line yake atakupa vipi na asimpe msanii wake. We utapita vipi? Ujinga unajizaa kwa style ya mapacha.

TID naye aliongeza, “now watangazaji sasa hivi wanatutukana and they can do anything to anyone wanaweza wakasema TiD amecopy wimbo bila ya research yoyote yaani anaweza kufanya kila kitu hana limit.”

Pia TID alieleza kuwa kama marehemu Mtoto wa Dandu aliyeanzisha tuzo za Kili angekuwepo, mambo yangekuwa tofauti.

“Kweli Dandu angekuwa Hai mimi Khaleeeed ningepata haki zangu zote I did a lot for this music…..and I inspired them a lot lakini hata concert ya Kuchangia huduma ya Maji hawataki niwepo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents