Habari

TID kortini kwa kujeruhi

TIDMSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khaleed Mohamed (TID) jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu tuhuma za kujeruhi. Tukio hilo lilitokea wiki iliyopita katika eneo la Slipway jijini Dar es Salaam.

TID


MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khaleed Mohamed (TID) jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu tuhuma za kujeruhi. Tukio hilo lilitokea wiki iliyopita katika eneo la Slipway jijini Dar es Salaam.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Jamal Rwambow alithibitisha kutokea kwa tukio hilo mwishoni mwa wiki iliyopita katika eneo la Slipway Dar es Salaam.


Rwambow alisema baada ya kutenda kosa hilo, TID alifunguliwa jalada la tuhuma
kwenye kituo cha Polisi Oysterbay na kushikiliwa kwa takriban saa 13 kabla ya kuachiwa na jana kufikishwa mahakamani.


“Ni kweli msanii huyo alikamatwa na kufikisha katika kituo cha Oysterbay akituhumiwa kumjeruhi kijana mmoja eneo la Masaki na leo (jana) amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma
hizo,” alisema Rwambow.


Gazeti hili lilimtafuta TID kupata ukweli juu ya tuhumu hizo ambazo alizithibitisha. “Ni kweli nilikamatwa na kupelekwa kituo cha Oysterbay kwa tuhuma za kumjeruhi mtu ambaye kwa kweli simjui na niliandika maelezo yangu na kuwekwa ndani kwa masaa karibia 13 ndipo nilifanikiwa kupatiwa dhamana,”alisema TID


Kwa mujibu wa TID, mtu anayedaiwa kumjeruhi alimtambua kwa jina moja la Ben na tukio
hilo lilitokea Julai 2. Hata hivyo, TID alisema alifikishwa mahakamani na yupo nje kwa dhamana hadi kesi itakapotajwa.


Hii si mara ya kwanza kwa msanii huyo kufikishwa mahakamani, siku za nyuma aliwahi kufikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma ya kumdhalilisha msichana,
lakini alishinda kesi hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents