TID Matatani Tena

TID Matatani Tena
Baada ya kutoka jela takriban miezi 6 iliyopita, msanii Khaleed Mohamed (TID) huenda akarejea tena gerezani…baada ya kurudia kosa kama lile lililomfunga mwanzo

Kwa mujibu wa gazeti moja litokalo mara moja kwa wiki,TID alitoa
mkong’oto huo mwishoni mwa wiki iliyopita (Ijumaa) usiku ndani ya Klabu
ya Thai Village, iliyopo Masaki.

Habari hizo zinalonga kuwa, katika kitwango hicho, pia mwanamuziki huyo
alizusha vurugu kubwa kwa kushika glasi za ‘ulabu’ na kuwamwagia wateja
waliokuwa katika jitihada za kuamulia timbwili hilo.

“Wakati tukimwamulia TID alitumwagia bia huku akidai kuwa, kama ni
Segerea ameshazoea, hakuna wa kumtisha,” kilidonoa chanzo hicho.

Kilisema kuwa, kipigo alichotoa mwanamuziki huyo kwa Naima ambaye ni
mwanafunzi wa shule moja jijini Dar kilikuwa kikubwa kwani
kilisababisha denti huyo atokwe na damu nyingi kichwani na puani.

Pia, ilidokezwa kuwa, mara baada ya kutoa kipigo hicho, msanii huyo aliingia mitini.

Ikaripotiwa kuwa, baada ya kuhisi ‘kimuhemuhe’ cha kipigo, Naima
alishika njia hadi Kituo cha Polisi cha Oysterbay na kumfungulia kesi
mwanamuziki huyo kwa namba ya faili RB/OB/10645/09 akidaiwa kufanya
Shambulio lenye kudhuru mwili.

Aidha, habari zaidi zinadai kuwa, mama mzazi wa mwanamuziki huyo baada
ya kupata ‘niuzi’ za mwanae kuachia ‘kitwango’ kwa mtu, tena demu na
‘vijana wa Mwema’ wanamsaka hadi chini ya kitanda aliangua kilio.

Wadaku wanadai kwamba, kilichomfanya mama TID aangue kilio ni baada ya
kukumbuka kuwa, kijana wake huyo alishatumikia kifungo cha mwaka mmoja
kwa kosa kama hilo na aliachiwa huru kupitia ‘samahani’ ya Rais JK
lakini akiwa ameshalala na kuamkia jela kwa miezi sita.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents