Michezo

Tiketi za pambano la Mayweather vs McGregor zaanza kuuzwa

Kuelekea pambano la ngumi ambalo linasubiriwa kwa hamu wadau wa mchezo wa Boxing kati ya Floyd Mayweather na Conor McGregor tayari tiketi za pambano hilo zimeanzwa kuuzwa huku Tiketi za bei ya chini zikiuzwa dola 2,013 za kimarekani sawa na Tsh milioni 4.5 .

Kwa mujibu wa mtandao wa waandaaji wa pambano hilo wa Show Time Boxing wameweka tiketi za pambano hilo kwenye viwango tofauti tofauti ambapo kiwango cha chini kikiwa ni Dola $2,013 huku Tiketi za bei ya juu zikiuzwa kwa Dola $93,609 ambayo sawa na Shilingi milioni 209 za kitanzania.

Pambano hilo ambalo watu wengi wataalamu wa masumbwi wamedai kuwa ni la kibiashara tuu sio la kiushindani zaidi kama lililovyokuwa lile la Mayweather dhidi ya Manny Pacquiao.

Pambano la Mayweather dhidi McGregor litafanyika Jumamosi ya Tarehe 26 mwezi Agosti mwaka huu huko Las Vegas nchini Marekani kunako ukumbi wa T-Mobile Arena.

Unaweza ukanunua na wewe Tiketi yako  HAPA  ili ukashuhudie pambano hilo la kukata na shoka .

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents