Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Timbulo ‘aduwazwa’ na Mo Music

Msanii Timbulo ameeleza kushangazwa na taarifa kuwa anambania Mo Music kurejea katika menejimenti yake ya zamani ambayo walikuwa pamoja.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha E-Newz cha EATV kuwa hawezi kufanya kitu kama hicho na alikuwa akitamani kumuona mbali zaidi kuliko alipo kwa sasa ila anaamini ipo siku atarudi kwenye nafasi yake.

“Yeye ndio azungumze Timbulo anambania wapi, kivipi, ila mimi ni moja ya watu ambao wakati Mo Music anajaribu kutoka kwenye menejimenti nilijaribu kumsisitiza na kumkataza asitoke, kwa hiyo kama leo anatamani kurudi ni kazi ya yeye na menejiment yake,” amesema.

Katika hatua nyingine amesema sehemu alipo Mo Music kwa sasa haendani nayo ukilinganisha na kazi ambazo amekwishakuzitoa na kufanya vizuri.

“Wimbo mmoja wa Mo Music ‘Basi Nenda’ alitakiwa aishi maisha yake yote kupitia ule wimbo lakini system haisapoti, kinachomkuta kwa sasa ni ups and down kitu ambacho hata mimi kilinikuta,” amesema.

By Peter Akaro

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW