Michezo
Timu tano Basketball Zathibitishwa
Timu tano za mchezo wa kikapu zimethibitisha kushiriki ligi ya kikapu mkoa wa Dar ,RBA.
Ligi hiyo inatarajiwa kuanza Novemba 27 katika uwanja wa ndani wa Taifa na Zanaki Dar es salaam. Akizungumza jana ,mkurugezi mtendaji wa mpira wa kikapu mkoa wa Dar es salaam, Mbaga Mwamboma alisema kwamba ‘Muda umebaki mfupi kabla ya tarehe ya mwisho’.
Alisema ligi hiyo ni muhimu kwa timu zote za Dar es salaam kwasababu ni sehemu pekee ya kupata wachezaji watakaoiwakilisha timu ya taifa ya Tanzania katika mashindano ya kimtaifa.
Alitaja timu zilizothibitisha kushiriki ligi hiyo kuwa ni pamoja na Vijana Stars,Police Dar es salaam, Pazi, na JKT Strs.