Habari

Timu ya Miami Heat yatwaa ubingwa wa mpira wa kikapu ‘2013 NBA Championship’ kwa mara nyingine

Kama wewe ni mfuatiliaji wa mchezo wa mpira wa kikapu wa Marekani NBA hii inakuhusu, timu ya Miami Heat imeibuka kuwa bingwa wa NBA kwa mwaka huu 2013.

Miami Heat

Wakiwa katika uwanja wa nyumbani (American Airlines Arena) Miami Heat jana Alhamisi (June 20) wamewagalagaza San Antonio Spurs kwa 95-88 na kuendelea kushikilia ubingwa kwa mara ya pili mfululizo.

Hii itakuwa ni mara ya tatu Miami Heat kuchukua ubingwa huo, mara ya kwanza ilikuwa (2006) na kufuatia mwaka jana (2012) na mwaka huu wameendelea kutetea ubingwa wao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents