Michezo

Timu ya Polisi yapokea vifaa tayari kwa mikiki mikiki ya ligi

Timu ya soka ya Jeshi la Polisi inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara imekabidhiwa vifaa na Benk ya NMB kwaajili ya maandalizi ya msimu ujao.

 

Meneja Mwandamizi kitengo cha wateja binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite (kushoto) akikabidhi vifaa kwa Naibu Kamishna wa Polisi, Adrian Magayane (kulia).

 Vifaa hivyo vyenye gharama ya shilingi milioni 13 ni pamoja na Jezi, viatu vya wachezaji, mipira, mabegi, na tracksuit za mazoezi.

Meneja Mwandamizi wa kitengo cha wateja binafsi wa NMB, Ally Ngingite amekabidhi vifaa hivyo kwa Kamishna wa Polisi, Adrian Magayane huku akisema kuwa vitendea kazi hivyo vitawasaidia katika michuano mbalimbali inayowakabili hususani ligi daraja la kwanza.

Baada ya kukabidhiwa kwa vifaa hivyo Kamishna, Magayane ameishukuru Benk hiyo kwa kuwapatia msaada wa vifaa ambavyo vitawaongezea chachu katika na hamasa katika mashindano yanayowakabili na kuhakikisha inafanikiwa adhima yake ya kutinga ligi kuu msimu ujao.

 By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents