Timu ya Taifa chini ya miaka 13 kwenda Ubeligiji

Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 13 (U13) inatarajia kushiriki michuano ya vijana itakayo kutanisha nchi zaidi ya10 kutoka mataifa mbalimbali yanayotarajiwa kufanyika Ubelgiji mwezi Agosti, 2018.

TFF inaandaa utaratibu sahihi wa kupata kikosi cha timu ya Taifa kwa vijana wenye umri huo ili kuweza kujiandaa na michuano hiyo ya vijana.

Ilikupata kikosi hiko kunatarajiwa kuchezwa mechi kati ya vijana wenye umri chini ya miaka 13 kutoka Tanzania Bara dhidi ya vijana wa Zanzibar katika siku za hivi karibuni ili kutoa nafasi kwa waalimu kuchaguwa wachezaji wenye vipaji watakaounda timu hiyo ya U13.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW