Michezo

Timu ya vijana ya Uingereza (U- 21) yatinga nusu fainali ya kombe la Ulaya

Timu ya taifa ya vijana ya Uingereza ya umri chini ya miaka 21 imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza tangu ilipofanya hivyo mara ya mwisho mwaka 2009 kwa kuifunga Poland ambao walikuwa pungufu uwanjani kwa jumla ya mabao 3-0 na kufanikiwa kuongoza kundi A.

England

Mchezaji wa klabu ya Leicester, Demarai Gray akifunga goli lake la kwanza

Mchezaji Demarai Gray ndio alianza kufunga goli katika dakika ya 6 ya mchezo huo  kabla ya kufanyiwa mabadiliko na kuingia Jacob Murphy ambaye naye alifunga bao la pili katika dakika ya 69 kisha mchezaji Lewis Baker alifunga goli la tatu dakika ya 82 kwa penati na kumaliza karamu ya magoli katika ushindi huo.

Mpaka sasa Uingereza bado haijajua timu itakayocheza nayo katika hatua hiyo ya nusu fainali mpaka itakapo malizika kwa michezo ya makundi siku ya Jumamosi. Huwenda timu hiyo ikakutana na timu za kundi B ambazo ni Ureno, Ujerumani, Itali au timu za kundi C ambazo ni Jamuhuri ya Czech na nyinginezo.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents