Aisee DSTV!
SwahiliFix

Timu zilizofuzu michuano ya CHAN Tanzania ikiwemo, Vigogo Senega, Ghana na Ivory Coast zashindwa kufuzu

Timu zilizofuzu michuano ya CHAN Tanzania ikiwemo, Vigogo Senega, Ghana na Ivory Coast zashindwa kufuzu

Ghana, Senegal na Ivory Coast zote zilishindwa kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika (CHAN) 2020 siku ya Jumapili. Ghana lishindwa kulipiza bao moja iliyofungwa katika mkondo wa kwanza dhidi ya Burkina Faso, na kutoka sare tasa mjini Ouagadougou.

Hii inamanisha kuwa Black Stars hawatashiriki fainali za mashindao hayo ya Cameroon 2020 ambayo yanachezwa na wachezaji wa Afrika katika mataifa waliozaliwa.

Senegal, pia ni timu kubwa ilioondolewa katika fainali hizo baada ya kushindwa na Guinea kupitia mikwaju ya penalti.

Senegal ilienda Conakry ikiwa kifua mbele na kwa bao 1-0 lakini Guinea ilijikakamua katika mechi yao ya nyumbani na kujipatia ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Mamadouba Bangoura.

Baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mechi zote, wenyeji walifuzu kupitia mikwaju ya penalti 3-1.

Ivory Coast ilishindwa kufuzu katika fainali hizo licha ya kushinda mechi yao ya nyumbani dhidi ya Niger 1-0.

Timu hiyo ilishindwa mabao 2-0 na Niger katika mkondo wa kwanza kumaanisha waliondolewa kupitia wingi wa mabao 2-1 .

Siku ya Jumapili pia, Zimbabwe ilijikatia tiketi ya kushiriki mashindano hayo ya Cameroon mwaka 2020 baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Lesotho lakini ikafuzu kwa wingi wa mabao 3-1.

DR Congo iliishabanga Jamhuri ya Afrika ya Kati mabao 4-1 mjini Kinshasa ushind ambao uliwapatia jumla ya mabao 6-1 huku nao Congo Brazzaville wakifuzu kwa bao 1-0 la nyumbani dhidi ya Equatorial Guinea na kunyakua jumla ya mabao 3-2.

Katika eneo la kaskazini,Tunisia ilijikatia tiketi ya mashindano hayo baada ya kupata ushindi wa jumla wa mabao 3-1dhidi ya Libya.

Mali pia itashiriki mashindano hayo baada ya Cameroon, baada ya kuinyuka Mauritania jumla ya mabao2-0.

Nigeria iliathiriwa zaidi katika mashindano hayo baada ya kushindwa na Togo siku ya Jumamosi huku bingwa watetezi Morocco wakipata ushindi dhidi ya Algeria.

Timu zilizofuzu kwa mashindano ya mataifa ya Afrika(CHAN) yatakayoandaliwa Cameroon:

 • Cameroon (mwenyeji)
 • Tanzania
 • Uganda
 • Rwanda
 • Zambia
 • Namibia
 • Togo
 • Morocco
 • Zimbabwe
 • DR Congo
 • Congo
 • Tunisia
 • Burkina Faso
 • Guinea
 • Niger
 • Mali

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW